Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Nipo kwenye harakati ya kuanzisha kakampuni kadogo, katakachoitwa ''equation x financial partnership''
Hiki kikampuni, kazi yake kubwa itakuwa ni kuingia ubia na wafanyabiashara wadogo wadogo (mama ntilie, boda boda, wauza genge n.k) ambao wako tayari kwenye biashara.
Kikampuni kitakuwa kinatoa fedha itakayotumika kununua 'stock', ambayo baadaye watauziwa walaji na fedha kupatikana; mfano, mama ntilie atawezeshwa fedha ya kununua nyama na mchele, na baada ya kuuza atarudisha rejesho na tutagawana faida.
Na hii project itaanza kwa mikoa mitatu; Dar, Arusha, Kilimanjaro.
Na kwa siku, kikampuni hakitatoa zaidi ya 50,000 kwa mjasiriamali mmoja; najua changamoto ni usimamizi wa marejesho, lakini tukiogopa 'risk' tutabaki kuwa masikini.
Kwa nini nimechagua hii; kwa sababu fedha itakuwa kwenye mzunguko na itakuwa inatengeneza faida kiasi pamoja na kutatua kero za wajasiriamali wadogo.
Kikampuni kitaingia nao (wajasiriamali waaminifu) makubaliano ya kimaandishi.
Nipeni maoni yenu kwenye hii biashara