Nipeni maoni yenu kwenye hii biashara

Equation x

JF-Expert Member
Joined
Sep 3, 2017
Posts
33,679
Reaction score
49,841
Nipo kwenye harakati ya kuanzisha kakampuni kadogo, katakachoitwa ''equation x financial partnership''

Hiki kikampuni, kazi yake kubwa itakuwa ni kuingia ubia na wafanyabiashara wadogo wadogo (mama ntilie, boda boda, wauza genge n.k) ambao wako tayari kwenye biashara.

Kikampuni kitakuwa kinatoa fedha itakayotumika kununua 'stock', ambayo baadaye watauziwa walaji na fedha kupatikana; mfano, mama ntilie atawezeshwa fedha ya kununua nyama na mchele, na baada ya kuuza atarudisha rejesho na tutagawana faida.

Na hii project itaanza kwa mikoa mitatu; Dar, Arusha, Kilimanjaro.

Na kwa siku, kikampuni hakitatoa zaidi ya 50,000 kwa mjasiriamali mmoja; najua changamoto ni usimamizi wa marejesho, lakini tukiogopa 'risk' tutabaki kuwa masikini.

Kwa nini nimechagua hii; kwa sababu fedha itakuwa kwenye mzunguko na itakuwa inatengeneza faida kiasi pamoja na kutatua kero za wajasiriamali wadogo.

Kikampuni kitaingia nao (wajasiriamali waaminifu) makubaliano ya kimaandishi.

Nipeni maoni yenu kwenye hii biashara​
 
Basi ofisi ziwe wazi mpaka saa 6 usiku. Maana ndiyo wengine watakuwa walau wamemaliza mauzo.
 
Basi ofisi ziwe wazi mpaka saa 6 usiku. Maana ndiyo wengine watakuwa walau wamemaliza mauzo.
Kutakuwepo na utaratibu maalumu ambao utakuwa rafiki kwa pande zote, na wasaidizi wangu ambao watakuwa 'front' nadhani mabinti au wajane wanaweza kufanya vizuri zaidi​
 
Aise hapana, bora uwe una supply raw materials (kama izo nyanya, hoho nyama kuku etc) ikifika jioni inainda kuokota maokoto, watu wengi wanafanya hizi biashara wengi vibati, sacossi na mikopo inamaliza ela za mtaji, unaweza ukampa 60000 za kwenye biashara akatoa 15000 akacheza kibati au ela ya rejesho
 
si mnasemaga "Kataa mdoa"
 
Umeona mbali sana, nadhani kama kutakuwepo na kipengele kwa mnufaika asiwe na mkopo wa aina yoyote, inaweza kusaidia zaidi; najaribu kufikiria kwa wale wasaidizi wangu kuwa karibu na hawa wahusika kimahesabu na uhakiki wa mauzo.​
 
Exactly, mwambie aandike list ya raw materials and then unamletea wewe unasubiri hela tu
 
Exactly, mwambie aandike list ya raw materials and then unamletea wewe unasubiri hela tu
Hii itafaa kwa hawa wenye magenge, ingawa nitakuwa nimejiongezea kazi/majukumu.
Ikiwa na maana kuchukua bidhaa kwa bei ya jumla, kuisafirisha (gharama) mpaka kwa muuzaji, pamoja na kupanga bei elekezi.
Hii itanipelekea kumiliki biashara yake yote, ambacho najaribu kukiepuka​
 
Ukiwa manage mama ntilies 100 tu ni hela ndefu per day. Wasumbufu hawakosi, obviously challenges are there to learn.

Hapo wakua nao uhakika ni wasimamizi tu. Lazima awe mtu anaye mjua mama ntilie na unamuamini.
 
Ukiwa manage mama ntilies 100 tu ni hela ndefu per day. Wasumbufu hawakosi, obviously challenges are there to learn.

Hapo wakua nao uhakika ni wasimamizi tu. Lazima awe mtu anaye mjua mama ntilie na unamuamini.
Ni kweli watu wanavyokuwa wengi usumbufu lazima uwepo, kwa mtazamo tu, hela utakayoiweka mwanzoni ndio hiyo hiyo itakuwa inajiendesha, muhimu tu mauzo yawe mazuri kwa siku.
Kama nguvu kubwa nitaweka kwenye kupata wasimamizi wazuri, nadhani biashara inaweza ikaenda vizuri; ingawa nawalenga wamama waliopitia magumu katika maisha, nadhani watakuwa na uchungu na kazi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…