Uchaguzi 2020 Nipeni miaka mitano muone maajabu

BAK

JF-Expert Member
Joined
Feb 11, 2007
Posts
124,790
Reaction score
288,165
Mwaka 2015 ulipewa miaka mitano na kwa kweli tumeona maajabu mengi.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu watumishi wa umma wakasota miaka mitano bila kupata nyongeza ya mshahara ambayo ni haki yao kisheria. Gharama za maisha zikapanda lakini kipato cha watumishi kikabaki kilekile. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia wahitimu wa kada muhimu kama udaktari na ualimu wakisota mtaani bila ajira lakini hospitali hazina madaktari na shule hazina waalimu. MAAJABU.

Tukashuhudia watu wa Kimara wakivunjiwa nyumba bila kulipwa fidia kwa kutumia sheria ya kikoloni ya mwaka 1932. Wakaenda mahakamani, na mahakama ikaweka zuio, lakini amri ya mahakama ikapuzwa na nyumba zikavunjwa. MAAJABU.

Tukashuhudia bunge likifanyiwa "shooting" kama bongo movie. Hotuba za wabunge zinakua censored kwanza. Walioongea maneno makali wanakatwa, walioipamba serikali wanaenda hewani. Bunge likapoteza focus na kuanza kuipongeza serikali wakati kazi ya bunge ni kuisimamia serikali. MAAJABU.

Tukashuhudia RC akivamia studio na mitutu ya bunduki kulazimisha "clip yake ya umbea" irushwe hewani. Chombo husika kikaamua kuzingatia maadili na kukataa kurusha clip hiyo. Waandishi wakavamiwa na kutishwa. Waziri aliyeunda Kamati ya kuchunguza suala hilo akafurushwa. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza mifuko ya hifadhi ya jamii ikafuta fao la kujitoa. Watumishi wa mikataba na wa muda mfupi wakaambiwa hadi miaka 60. Mtu mwenye akiba ya 5M na kwa sasa ana maika 25 unamwambia hadi afikishe miaka 60? Yani miaka 35 ijayo? Akifikisha miaka 60 hiyo 5M si itakua ya kununulia mkate tu? MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia Hakimu aliyekua kwenye likizo ya kustaafu akiteuliwa kuwa Jaji wa mahakama kuu. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia mbunge akipigwa risasi kwenye makazi yenye CCTV camera. Lissu akasema camera ziliondolewa baada ya tukio. Hakuna mshukiwa hata mmoja aliyekamatwa hadi sasa. MAAJABU.

Tukashuhudia mikutano ya siasa ikipigwa marufuku kinyume na katiba na sheria za nchi. Viongozi wa upinzani walipofanya vikao vya ndani walikamatwa lakini CCM walifanya mikutano ya hadhara na vikao bila bughudha. MAAJABU.

Binafsi naona maajabu yametosha baba. Hatutaki maajabu mengine.!

Malisa GJ
 
Mmepata Rais Jiwe Kweli Kweli Hatishwi 😅😀😁😂😃🤣
 
IMG-20200905-WA0043.jpg
 
Unamkubali vipi dhalimu anayependa kuwanyanyasa, kuwadharau, kuwadhalilisha na kuwatukana Watanzania. HAFAI huyu!

Huyu bwana wengi tumemkataa toka moyoni.
acha twende na lisu.
 
Pamoja na yote bado atapita tu.
Hakuna mtu asiyekuwa na madhaifu
Asante...

Hatutakuja kupata kiongozi Mungu.

Ila wapinzani waache wapnge maana kupinga ndiyo uhai wao. Waendelee tu.

Kipindi cha Mkapa walilalamika Rais dikteta hafai kututawala.

Akaja JK tukamsema huyu kageuza nchu shamba la bibi. Tu/wakatamani kiongozi mwenye mamlaka. Anayeweza kunguruma kidogo.

Akaja JPM...malalamiko hayajaisha. Rais ni mtu sio Mungu. Lazima wawepo wa kuumizwa na wa kufurahishwa na maamuzi anayotoa.
 
Nyie chadema mna bangi kweli. Hivi utawaongezea mishahara wafanyakazi alafu serikali iache kuwekeza kwenye miradi Ambayo itakuja kuwa mkombozi kwa wananchi WOTE?

Hivi kupi ni bora kuwekeza kutakapo kuja kukupatia kipato kitakacho kuwezesha kujikimu na kuhudumia familia yako vizuri.

Au Bora kula kipato chote unachokipata pasipo kuwe keza?

Unaposema serikali haija Ajiri watumishi katika sekta je! Ni Vyema kuajiri lundo la wafanyakazi Ambao hutaweza kuwalipa vizuri?

Chadema WOTE Akili zao ni Ndogo sana Mna zani kuongoza nchi ni sawa na kuongoza kijiwe cha kahawa.

Nyinyi ni vipofu na hamjui Impact ya Serikali ya Awamu ya 5 kwa Kazi kubwa iliyofanya Mtakuja kuona Hapo Baadae wakati mmeshapata Akili.
 
Kwa nini EU na merekani na inchi zingine za ulaya mabalozii wao hawatoi matamko tena kuwaonya chadema na act wazalendo juu ya kufunya mikutano yenye misururu ya watu kwa kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa korona?
Mbona wako kimya saanaa?
Au nawao wanaamini Tanzania hamna korona kama magufuli ambavyo anaamini??
 
Nyie chadema mna bangi kweli. Hivi utawaongezea mishahara wafanyakazi alafu serikali iache kuwekeza kwenye miradi Ambayo itakuja kuwa mkombozi kwa wananchi WOTE?

Hivi kupi ni bora kuwekeza kutakapo kuja kukupatia kipato kitakacho kuwezesha kujikimu na kuhudumia familia yako vizuri.

Au Bora kula kipato chote unachokipata pasipo kuwe keza?

Unaposema serikali haija Ajiri watumishi katika sekta je! Ni Vyema kuajiri lundo la wafanyakazi Ambao hutaweza kuwalipa vizuri?

Chadema WOTE Akili zao ni Ndogo sana Mna zani kuongoza nchi ni sawa na kuongoza kijiwe cha kahawa.

Nyinyi ni vipofu na hamjui Impact ya Serikali ya Awamu ya 5 kwa Kazi kubwa iliyofanya Mtakuja kuona Hapo Baadae wakati mmeshapata Akili.
Wengine waliwezaje kwanj i yeye afeli. Ai kukosa mahesabu na kukurupuka??
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Mwaka 2015 ulipewa miaka mitano na kwa kweli tumeona maajabu mengi.

Kwa mara ya kwanza katika historia ya nchi yetu watumishi wa umma wakasota miaka mitano bila kupata nyongeza ya mshahara ambayo ni haki yao kisheria. Gharama za maisha zikapanda lakini kipato cha watumishi kikabaki kilekile. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia wahitimu wa kada muhimu kama udaktari na ualimu wakisota mtaani bila ajira lakini hospitali hazina madaktari na shule hazina waalimu. MAAJABU.

Tukashuhudia watu wa Kimara wakivunjiwa nyumba bila kulipwa fidia kwa kutumia sheria ya kikoloni ya mwaka 1932. Wakaenda mahakamani, na mahakama ikaweka zuio, lakini amri ya mahakama ikapuzwa na nyumba zikavunjwa. MAAJABU.

Tukashuhudia bunge likifanyiwa "shooting" kama bongo movie. Hotuba za wabunge zinakua censored kwanza. Walioongea maneno makali wanakatwa, walioipamba serikali wanaenda hewani. Bunge likapoteza focus na kuanza kuipongeza serikali wakati kazi ya bunge ni kuisimamia serikali. MAAJABU.

Tukashuhudia RC akivamia studio na mitutu ya bunduki kulazimisha "clip yake ya umbea" irushwe hewani. Chombo husika kikaamua kuzingatia maadili na kukataa kurusha clip hiyo. Waandishi wakavamiwa na kutishwa. Waziri aliyeunda Kamati ya kuchunguza suala hilo akafurushwa. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza mifuko ya hifadhi ya jamii ikafuta fao la kujitoa. Watumishi wa mikataba na wa muda mfupi wakaambiwa hadi miaka 60. Mtu mwenye akiba ya 5M na kwa sasa ana maika 25 unamwambia hadi afikishe miaka 60? Yani miaka 35 ijayo? Akifikisha miaka 60 hiyo 5M si itakua ya kununulia mkate tu? MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia Hakimu aliyekua kwenye likizo ya kustaafu akiteuliwa kuwa Jaji wa mahakama kuu. MAAJABU.

Kwa mara ya kwanza tukashuhudia mbunge akipigwa risasi kwenye makazi yenye CCTV camera. Lissu akasema camera ziliondolewa baada ya tukio. Hakuna mshukiwa hata mmoja aliyekamatwa hadi sasa. MAAJABU.

Tukashuhudia mikutano ya siasa ikipigwa marufuku kinyume na katiba na sheria za nchi. Viongozi wa upinzani walipofanya vikao vya ndani walikamatwa lakini CCM walifanya mikutano ya hadhara na vikao bila bughudha. MAAJABU.

Binafsi naona maajabu yametosha baba. Hatutaki maajabu mengine.!

Malisa GJ
Hatutaki maajabu hasi
 
  • Nzuri
Reactions: BAK
Back
Top Bottom