Elections 2010 Nipeni mitano mingine 'nifunike' zaidi-Kikwete

Elections 2010 Nipeni mitano mingine 'nifunike' zaidi-Kikwete

Mmh! Kumbe mitano iliyopita amefunika? Kwa kubwa lipi? Mbona hali zetu wadanganyika zimezidi kuwa mbaya? Mitano mingine si ndiyo tutapotea kabisa kwenye ramani jamani au ndo kama alivyosema 'atufunike'-atufukie kabisa?
 
"kufunika" sound like oxymoron like 'sharp dull'
 
alidai hii mitano alikuwa anajifunza na kafanya yote hayoo, akiongezewa mitano zaidi itakuwajeee?? aliuliza.

ila desemba 30, 2005, alisema, mafanikio ya awamu ya tatu ni makubwa, tutajitahidi ya kuyaendeleza, na hata kiatu kisipokutosha unaweka majani!!! tehe tehe...
 
Miaka 3 ya kujifunza na kufanya semina angalizi; Kusafiri na kuijua dunia, Miaka miwili ya kuandaa timu ya ushindi; Miaka mingine mitano ya kujiandalia 'mafao ya uzeeni' na kuandaa mtu wa 'kupokea' kijiti teh teh teh
 
hapa anamaanisha afunike macho yaani afumbe macho mafisadi wazidi kuitafuna Nchi yetu
 
huyu nae alisha nikatisa tamaa sana
 
Du. Kumbe jamaa alikuwa anajifunza!!!! Mbona wakati anaomba kazi hii mwaka 2005 hakusema kuwa anaomba urais ili akajifunze? Kumbe ilikuwa miaka ya kasi mpya , ari mpya na nguvu mpya ya kujifunza? Katika kujifunza kuna kufaulu au kushindwa. Mi naona kama kweli alikuwa anajifunza miaka 5 iliyopita basi amefeli masomo na inatakiwa a"DISKO" siyo "supplimentary". Huwezi kwenda kujifunza ikulu!!!!!!!! Mambo gani haya jamani
 
Yaani tangu alipopewa unaibu waziri wa madini, fedha, mambo ya nje alikuwa hajajifunza bado? unawezaje kwenda vitani hujui hata trigger ya bunduki iko upande upi na unafanyaje ili kutumia bunduki? Huu ni upuuza, dharau na matusi ya hali ya juu kwa wananchi.
 
Back
Top Bottom