HUZUNI-ka: grief, sorrow, mourning, distress, dolour= Hii hufuata na machungu moyoni. Inachukua muda mrefu kumliwaza mwenye huzuni.
SIKITI(KO)-ka: Sadness, disappointment, regret = Kutokuwa na furaha; kutoridhishwa na hali au tabia, kujuta au kujutia.
Mifano:
- Kifo cha baba yake kilituhuzunisha sote. Hapa mfiwa na wengine huwa na huzuni.
- Inasikitisha kumwona jinsi anavyolewa hadi kuaibika. Pengine hata mlevi mwenyewe hana masikitiko juu ya matendo yake.
- Jana nilikupa pesa, leo unataka tena. Nasikitika, leo siwezi kukusaidia. Hapa inaonesha kuvunjika moyo zaidi kuliko kusikitika.
- Unasikitika nini? Ninasikitika gari nimenunua mwaka jana tayari imeanza matatizo.