Nipo Njiani kuelekea kwenye upambanaji ushauri wako boss ni wa muhimu

Smith Rowe

JF-Expert Member
Joined
Sep 18, 2018
Posts
4,319
Reaction score
9,003
Tuache propaganda tujikinge na Corona

Moja kwa moja kwenye mada!!!

Mimi ni kijana wa miaka 20 bado Niko darasani ila natumai baada ya kumaliza kidato cha sita nitafanya biashara kwanza kabla ya kuendelea na masomo.

Hipo hivi!!
Mimi ni mkazi wa Mkoa mmoja wapo wa kaskazini. Nategemea kuanzisha uzalishaji mdogo wa SEMBE (mtaji wa 2M)Kwa utaratibu ufuatao:

1.Sitakodisha pango wala kununua mashine ya ukoboaji maana mtaji ni mdogo bali ntakua nikikoboa na kusaga kwenye mashine ya mtu.

2.Sitatafuta usajili wa business name maana mtaji ni mdogo.

3. Naomba maelekezo wapi yanapatikana mahindi yenye mbegu ndogo mikoa ya kaskazini kwa uzalishaji wa sembe.

4.Naomba maelekezo wapi vinapatikana vifungashio vya unga vya bei nafuu vya kilo moja, tano na kumi kwa mikoa ya kaskazini

5. Naomba ushauri juu ya gharama za uzalishaji wa Sembe.

6. Naomba ushauri wa masoko na mauzo ya unga wa sembe .

7. Naomba ushauri juu ya ufungishaji wa sembe kwenye mifuko yake.

8.Naomba ushauri juu ya uzoefu wa biashara hii na jambo lolote litakalonisaidia kuifanikisha.

Nitashukuru kwa msaada wenu wa mawazo pamoja na mkoa mmoja wapo wa kufanya hii biashara kati ya mmkoa mmoja wapo wa kaskazini ( mwanza,arusha,shinyanga,moshi) au popote pale patakapo kuwa panafaa zaidi.

Karibuni wadau kwa ushauri

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kila la kheri mkuu!! Wadau ktk sekta hiyo wanakuja..... Ila kwa Sasa debe la Mahindi Ni 7500 Hadi 8000 kwa Kigoma!!
 
Wazo zuri hili, ngoja waje kukupa mwongozo.
 
Mbona uanulizia mbegu??? [emoji1787][emoji1787][emoji1787] Achana na kilimo ndugu, Nunua mahindi kisha process uuze unga

Emaphakadeni
 
Hongera mpendwa..pambana
 
Uko wapi? Make moja ya Changamoto ya hii biashara ni kwamba Competition ni kubwa sana, Brand ni nyingi sana na ukiachilia brand unakutana tena na Washindani binafidi yaani wengi huenda kusaga unga mashineni,

Ndo maana kama ni city centre ni sawa ila kwa mawilayani huko bado mindset ni za kwenda mashineni kusaga unga wa kupika.

Vifungashio Kwa Kaskazini watafute Harsho hawa wako Moshi wanatengeneza kila aina ya vifungashio yaani mifuko, sina contact zal ila unaweza watafute kwa search engene, Harsho Group
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipo moshi

Soko langu nategemea iwe ni moshi mjini

Harsho nawajua na nategemea kwenda hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…