Nipo tayari hapa Halmashauri kupokea walimu wapya 3 nilioahidiwa lakini....

Wazo la kabwela

JF-Expert Member
Joined
Feb 13, 2013
Posts
1,812
Reaction score
1,373
tayar nimeshafika hapa katika ofisi za halmashaur.nipo karibu kabisa na ofisi za idara ya ELimu.mimi si mwalimu mpya laa hasha mimi huu ni mwaka wangu wa tatu kazini.lengo la kuja hapa ni kupokea walimu wapya 3 tulioahidiwa kuwapata katika shule yetu.kwa haraka haraka nawachunguza walimu wetu wageni na kugundua yafuatayo.
1.walimu wa kiume wapo tyari kufanya kazi popote watakapopangiwa.
2.walimu wa kike sasa..
hawa wamekaa katika vikundi wakijadiliana huku weng wakiwa na nyuso za huzuni inaonyesha tyar wameshakata tamaa.
kitu kingine ni jinsi walivyojiremba.. kucha za bandia,nyusi za bandia na mawigi.Hapa ndo napoanza kuwaonea huruma dada zangu hawa coz huko vijijini watajikuta wanavisahau vyote hivyo na ninategemea kuwaona tofauti kabisa mwisho wa miezi katika kuchukua mishahara kwani kuna vijiji vinatisha jamani uwii nawaonea huruma hawa dada zetu
 
Bila shaka utakuwa ni mwalimu katika shule ya sekondari Biro,Malinyi,Ulanga,Morogoro maana huko ni hatare;i.e.1.Usafiri ni utata mtupu unavuka mito kwa kupiga mbizi ukipishana na mamba 2.Mtandao wa simu ni mpaka ukwee mnazi ndo unapata kwa mbaalii 3.Kipindi cha mvua na kilimo mahudhurio ya walimu na wanafunzi ni zero 4.Hakuna huduma muhimu za jamii!5. Uchawi ni motoo,hata watoto wachanga wachawi! NB:Huku ni nyumbani kabisa kwa Mh Ngasongwa.
 
Ha ha! Eti wanahuzuni !! Umeniona miye nimevaa pedo na wigi kubwaa!!
 
Bila shaka utakuwa ni mwalimu katika shule ya sekondari Biro,Malinyi,Ulanga,Morogoro maana huko ni hatare;i.e.1.Usafiri ni utata mtupu unavuka mito kwa kupiga mbizi ukipishana na mamba 2.Mtandao wa simu ni mpaka ukwee mnazi ndo unapata kwa mbaalii 3.Kipindi cha mvua na kilimo mahudhurio ya walimu na wanafunzi ni zero 4.Hakuna huduma muhimu za jamii!5. Uchawi ni motoo,hata watoto wachanga wachawi! NB:Huku ni nyumbani kabisa kwa Mh Ngasongwa.

nipo mpwapwa kwa mh. SIMBACHAWENE mkuu ni shidaa
 
tayar nimeshafika hapa katika ofisi za halmashaur.nipo karibu kabisa na ofisi za idara ya ELimu.mimi si mwalimu mpya laa hasha mimi huu ni mwaka wangu wa tatu kazini.lengo la kuja hapa ni kupokea walimu wapya 3 tulioahidiwa kuwapata katika shule yetu.kwa haraka haraka nawachunguza walimu wetu wageni na kugundua yafuatayo.
1.walimu wa kiume wapo tyari kufanya kazi popote watakapopangiwa.
2.walimu wa kike sasa..
hawa wamekaa katika vikundi wakijadiliana huku weng wakiwa na nyuso za huzuni inaonyesha tyar wameshakata tamaa.
kitu kingine ni jinsi walivyojiremba.. kucha za bandia,nyusi za bandia na mawigi.Hapa ndo napoanza kuwaonea huruma dada zangu hawa coz huko vijijini watajikuta wanavisahau vyote hivyo na ninategemea kuwaona tofauti kabisa mwisho wa miezi katika kuchukua mishahara kwani kuna vijiji vinatisha jamani uwii nawaonea huruma hawa dada zetu

Kwako Mpendwa Mwalimu mwenye uzoefu wa Miaka Mitatu katika Kazi ya Ualimu,

Mosi, asante sana kwa kutujulisha kuwa wewe umepewa dhamana ya kwenda kwenye Ofisi za Halmashauri ya Wilaya yenu kwa madhumuni ya kupokea Waalimu wapya waliopangiwa kufanya Kazi Shuleni kwenu.

Pili, kwa niaba ya Wapenzi wa Uandishi wa Kiswahili fasaha hapa Jamvini, ambao wengi sio Waalimu kama wewe, ninachukua nafasi hii, kujaribu kuandika upya ulichokiandika hapo juu, ili Wasomaji wenye ufahamu waweze kusoma kwa starehe na kuelewa ulichonuia kukiandika:

"Wakuu Wanajamvi, nimekwishafika hapa katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya. Niko karibu kabisa na Ofisi za Idara ya ELimu. Mimi si Mwalimu mpya, la hasha! Huu ni Mwaka wangu wa Tatu Kazini. Lengo la kuja hapa, ni kupokea Walimu wapya Watatu tulioahidiwa kuwapata katika Shule yetu. Kwa haraka haraka ninawachunguza Walimu wetu wageni na ninagundua yafuatayo:
1. Walimu wa Kiume wako tayari kufanya Kazi popote watakakopangiwa
2. Walimu wa kike sasa...! Hawa wamekaa katika Vikundi wakijadiliana, huku wengi wakiwa na nyuso za huzuni. Inaonyesha tayari wamekwishakata tamaa. Kitu kingine ni jinsi walivyojiremba... kucha za bandia, nyusi za bandia, nywele za bandia (mawigi), n.k. Hapa ndio ninapoanza kuwaonea huruma Dada zangu hawa, kwa sababu huko Vijijini watajikuta wanavisahau vyote hivyo. Ninategemea kuwaona wakiwa tofauti kabisa mwishoni mwa Miezi wakati wa kuchukua Mishahara, kwani kuna vijiji vinatisha jamani! Uwii! Ninawaonea huruma hawa dada zetu!"

Ninaamini sio kosa lako Mwalimu, ni tatizo la Simu za Viganjani vilivyotengezwa India na Pakistan.

Wasalaamu
 
Hahahahaha,!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
Kweli kabisa,kuna dada yangu alipangwa shule moja ya msingi inaitwa Shule ya msingi Katunguru,iko kandokando ya ziwa Viktoria wilaya Muleba mkoa wa Kagera.Barabara hamna,umeme hamna,shule yenyewe ilkua chakavu(mwaka 2000).Ila watu wake walikua wakarimu na wafuasi wa elimu.
 
kwa hiyo wewe ulivosema unachukua nafasi ni kiswahili sahihi sio.
 
Ni kibakwe mkuu sio mpwapwa kijiji gani umepangiwa?

Kibakwe ni moja ya majimbo mawili yaliyo katika wilaya ya mpwapwa.jimbo la mpwapwa na jimbo la kibakwe.kibakwe ni jimbo sio wilaya nadhani umenielewa mkuu?.
 
Back
Top Bottom