Nipo ugenini, wanapika chakula kidogo mno

Live circuit

Senior Member
Joined
Mar 11, 2023
Posts
124
Reaction score
365
Huu ugeni jamani,

Nipo ugenini hapa nilipofikia nimejitahidi nisiwe nakula bure, nimefika ijumaa na Ile Ile ijumaa nilileta mafuta ya kula Lita 3.

Hapo hapo nikanunua na nguruwe kilo 2, huwa sipend Sana free lunch. Sasa bana hapa nilipo wanapika msosi kidogo sana yaani daah sijui ndo walivozoea.

Daah nakula slow slow Ila sishibi. Ijumaa na jumamosi nimekula sahani mbili tu yaani mchana napiga chenga, sipendi kuhudhuria kila mida ya misosi.

Sasa Leo jioni (muda si mrefu sijaanza kuandika hii post) Wife wa jamaa wakaleta msosi kama kawaida yao kidogo sana. Nimekaa nazuga zuga naangalia TV uvumilivu ukanishinda nikaona ngoja nimege ugali.

Nikakata nusu, maana nilijua tupo wawili mi na jamaa mwenye nyumba. Nikahisi wife wa jamaa na mdogo wake wanakula uko jikoni. Ile nimekata nusu naona wife wa jamaa na mdogo wake nao Wanakuja daah!

Basi shem ikabidi azuge kama kashiba. Mdogo wa Shem ndo akakata Ile nusu, uliobaki ndo jamaa kala. Nimejisikia vibaya mno natamani niondoke Lee. Yaani jumatatu naona mbali.
 
Ishu za misosi mara nyingi ukiwa ugenini inabidi ujinyime flani hivi.

Apo inabidi uwe na mpango wa kando unakula mgahawan uko ukija ukirudi Hapo unajaziajazia fresh siku inaenda.

Hakuna kitu kigumu Kama uwe ugenini alafu ukute Aina yao ya maisha hujazoea Kabisa Aisee!!

Kama hakuna ishu ya muhimu ya kukuweka Hapo ni Bora uage usepe walau ukakae lodge Hadi umalize Mambo yako.
 
๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚๐Ÿ˜‚ pole sana, mjini bajeti mzeee
 
Aseee! Hiyo kawaida kabisa, hutokea watu wengi sana. Sisi watu wa kusini tumezoea kujaza sahani maana misosi yakutosha, hao wa Dar Wana budget Kali sana. Ila kama unamishe zako si vema sana kufikia Kwa ndugu ama jamaa, panga budget yako vema ili ufikie lodge ya Bei unayoimudu.
 
Kuna siku nilikuwa na wageni Fulani watasha sehemu Fulani, wao wanakula Kidogo sana, Mimi nikamsoma dereva maana mswahili mwenzangu, yeye anajifanya anazuga alafu anaaga anaenda kufata vocha aloo Kumbe anaenda kwenye mgahawa wa karibu na kupiga mapigo ya kibongo. Niliunga tela fasta siku inayofata nikamwambia na Mimi nataka nitume M-pesa sehemu akaniambia njiani asee Mimi huwa sishibi hiyo misosi nikamwambia sio peke yako, alicheka sana. Nikaagiza ugali sahani mbili chap, dereva alicheka sana. Hii ndio mipango. [emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ