Nipongeze Serikali kwa jitihada za Viwanda

Nipongeze Serikali kwa jitihada za Viwanda

Kamundu

Platinum Member
Joined
Nov 22, 2006
Posts
7,823
Reaction score
10,857
Lazima tuweke utamaduni wa kupongeza. Uwekezaji umeongezeka na kwenye hili hakuna ubishi. Lakini cha kufurahisha ni kwamba uwekezaji umeongezeka wakati bado kuna Covid. Hii imetokana na uwezo mkubwa wa mawasiliano kutoka juu yaani Raisi wetu amekuwa mtu mzuri kwa mawasiliano ukilinganisha na huko nyuma. Huko nyuma tulikuwa tunaongelea wawekezaji lakini tulikuwa tunawaona wawekezaji wa nje kama wezi au mabeberu!. Tumegundua kwamba kujigamba gamba pekee haitoshi na hapa ni lazima tupongeze tunaona kwa itendo kabisa viwanda vinafunguliwa.

Lakini nitoe ushauri. Kuna sehemu bado inabidi turekebishe

1. Bank kuu bado haifanyi vizuri. Inabidi itungwe sheria kuhakikisha ajira ipo kwenye agenda za bank kuu. Lakini hatuna sababu ya mikopo mpaka leo kuwa 15%-24% hii inapunguza sana uwekezaji. Na tatizo ni kwamba wakuu wa bank zetu wana nguvu kuliko gavana na gavana wetu ni kama hawezi kabisa kukabiliana na hawa viongozi wa bank na kushusha riba za juu za mikopo
2. Lazima tuongeze uwekezaji kwenye Utalii hasa Kilimanjaro, Arusha, Manyara na Zanzibar.

Mfano Kwa Arusha na Manyara serikali iwekeze kwenye Mall/ Soko kubwa la kuuza vitu vya sanaa. Hii itasaidia jamii ya wamassai kuuza vitu vya sanaa badala ya kutegemea ufugaji zaidi. Lakini soko tayari lipo watalii wanapenda kununua vitu vya sanaa lakini haviko vya kutosha. Lakini sehemu ya makumbusho ambayo watalii wakifika wanaweza kwenda na kujua historia ya nchi yetu badala ya kusoma mitandaoni.

3. Chuo cha teknologia ambacho Raisi anakipigania kije kwa kasi. Lakini vyuo tayari vipo vingi ni kubadilisha vyuo kuendana na wakati. Kijana akijua sofware anaweza kufanya kazi za nje.

4. Hii ni kwa Raisi Samia ukitaka twenda haraka wafanye wapinzani wadau badala ya maadui kuna watu wengi sana wanafaidika na kuwanyanyasa wapinzani lakini haisaidii taifa bali watu binafsi. Hii haina tofauti na rushwa. Hauwezi kufanikiwa vizuri kama 40% ya watu unawaona kama wahasi badala ya watani. Kama wapinzani wana nia ya maendeleo kupingwa na kupigwa vijembe ni muhimu kwa taifa kwasababu ni kwa manufaa ya taifa.

Agalia kwenye mitandao Magufuli anakumbukwa kwa mabaya zaidi kutokana na aliyowafanyia upinzani. Usiende huko hili liwe fundisho. Kwenye biashara kuna ushindani, kazi zina ushindani, michezo ina ushindani hata nchi zina ushindani sasa kwanini siasa ushindani uwe uhasama!
 
Back
Top Bottom