Nisaidien Jamani!!!

Jasho la Damu

JF-Expert Member
Joined
Mar 10, 2011
Posts
956
Reaction score
120
Mimi ni kijana wa kiume nina umri wa miaka 24 nafanya kazi ktk ofisi ya Serikali nisingependa kuitaja kwa usalama wangu. Nimekuwa nikisumbuliwa na bosi wangu wa kike aliyenizidi miaka 9 kiumri na amezaa mtoto mmoja wa kiume lkn hana mume. Bosi huyu anitaka kimapenzi na siku zote huwa ananifanyia visa vya ajabu, utakuta ananitumia msg za ajabu usiku eti anaomba nimpeleke Soda moja na mayai mawili ana hamu nayo sana. Mara nyingine huwa ananipa kazi mpaka jioni ili tubaki wawili tu ofisini na kuanza visa vyak
 
kama mnavyofahamu kazi za Serikali uishia saa tisa na nusu lkn yeye unipa masaa ya nyongeza na kunihaidi kuwa atanilipa. imekuwa ni desturi yake kufanya hivyo lkn nimekuwa nikimpotezea tu ikafikia hatua ananiita ofisini kwake na unishikashika mikono na kuniambia ananipenda na anafurai mimi kuwa mtumishi katika ofisi yake. lkn sasa mambo yamebadilika tangu alipogundua kuwa nataka kuoa, hanipi kazi na hata nikimsalimia haitikii.kazi sasa naiona chungu. naomba ushauri wenu jamani.
 
Pole kijana ndo utu uzima huo. Huyo mchumba wako anajua kama huyo mama anakutaka? kama hajui me nakushauri rudi kwa huyo bosi wako mkubalie hlf mpe mambo kisawa sawa yaani msugue haswa ikiwezekana unywe vile vinywaji vyetu ndo uingie nae kwenye mechi akitoka hapo anakukabidhi mafaili yote ya ofisi wewe ndo unakuwa bosi. Usichezee bahati mdogo wangu itumie hiyo uwe tajiri.
 
acha zako za kimasai bana,........mpende akupendae na siyekupenda,.........
 
hiii nayo ni shida ya kuomba ushauri????????

siku hizi wanaume wanazidi kupungua,wanabaki wavulana tu naona
 
Kuwa makini waweza poteza kazi ndg sijui utaishije? 24+9=33 Mh! Kazi kwelikweli
 
kimbia wala usiangalie nyuma; ikimbieni zinaa
 
Niunganishe naye mimi ataacha kukusumbua
 
Mchumba wangu bado hajajua. ila kaka ushauri wako huu dah anyway i respect u.
 

Kwel wewe ni mwanaharakat! Lol.,. Kumbe hii nayo ni bahati eeh? Akipata na UKIMWI JE???
 
Duh, ushauri mwingine utafikiri unatoka kuzimu!!!
 
analipa huyo boss? asije akawa kama yule wa Bungeni pale sijui spika sijui nani?
 
Huyo boss we mpotezee tu wala asikutishe na cheo chake. Just imagine ndo wewe sasa unamkuta mchumba wako umpendae anakusaliti na kuamua kuzini na boss wake! Utajisikiaje??
 
Mkuu, wafanyakazi wote wa Serikalini bosi wao ni serikali kupitia mgt ya utumishi wa uma. Kwa kusema hivyo nina maana huyo Boss wako sio muajiri wako hivyo hawezi kukufukuza kazi. Suala la mapenzi ni la mtu binafsi hivyo kama haumpendi hakuna aja ya kujilazimisha kumpenda eti kwa sababu ni boss wako, inavyotakiwa ni kuwa ktk maadili ya kazi kila wakati kama unahofia kulimwa vi memo, kisha kama utaonewa kufukuzwa kazi si utawasilisha utetezi wako. Jihadhari na mashuga mami mengine yameshanasa yanataka kuongeza idadi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…