Nisaidieni hili neno

Nisaidieni hili neno

SHIEKA

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2011
Posts
8,240
Reaction score
4,265
Enyi wataalam wa Kiswahili. Naomba msaada wa hili neno: Noma. Najua maana yake lakini hapa JF neno hili huandikwa kwa spelling tatu tofauti kama: 1. noma 2.nouma 3noumer Mimi najua spelling namba 1 ndiyo sahihi hasa ila namba 2 na 3 ni spelling ya kifaransa na kutamka ni numa kwa namba 2 na 3. Je huu ni upotoshwaji wa bahati mbaya au makusudi? Na madhumuni yake ni nini? Nawashukuru
 
Tuambie kwanza maana unayoijua wewe, pengine upo/haupo sahihi.
 
Enyi wataalam wa Kiswahili. Naomba msaada wa hili neno: Noma. Najua maana yake lakini hapa JF neno hili huandikwa kwa spelling tatu tofauti kama: 1. noma 2.nouma 3noumer Mimi najua spelling namba 1 ndiyo sahihi hasa ila namba 2 na 3 ni spelling ya kifaransa na kutamka ni numa kwa namba 2 na 3. Je huu ni upotoshwaji wa bahati mbaya au makusudi? Na madhumuni yake ni nini? Nawashukuru

.

Hivi kweli wewe unajua maana ya neno Noma?!

Unajua watu wengi hufikiri kuwa neno Noma ni la vijana na limekaa kama la mtaani! na hata wewe unasema unajua maana yake!

Hili ni neno la kiswahili FASAHA Ndio maana hata kwenye Kamusi ya TUKI lipo hili neno na lina maana 2

noma
[SUP]1[/SUP] nm [i-/zi-] work chit (as a proof that one was working)

noma[SUP]2[/SUP] nm [i-/zi-] obstacle, objection:

Mfano: Sina noma mie - I have no objection.

Neno lingine ambalo watu hulichukulia kama la mtaani ni Nomi! .... (nyomi)

Tatizo lililotokea hapa ni kuwa watumiaji wanakosea badala ya kusema Nomi baadhi wanasema Nyomi! Mfano utakuta mtu anapiga stori alafu anasema 'katika mkutano hou watu walikuwa Nyomi (Nomi)

Katika Kamusi ya TUKI wameeleza maana ya neno NOMI

nomi kl in abundance: Machungwa yamejaa NOMI ----- oranges are in abundance.

Ahsantee mkuu meipenda nilikua najjua moja tu ya objections bt hiyo in abundance nilikuwa sijui.
 
Back
Top Bottom