.
Hivi kweli wewe unajua maana ya neno Noma?!
Unajua watu wengi hufikiri kuwa neno Noma ni la vijana na limekaa kama la mtaani! na hata wewe unasema unajua maana yake!
Hili ni neno la kiswahili FASAHA Ndio maana hata kwenye Kamusi ya TUKI lipo hili neno na lina maana 2
noma[SUP]1[/SUP] nm [i-/zi-] work chit (as a proof that one was working)
noma[SUP]2[/SUP] nm [i-/zi-] obstacle, objection:
Mfano: Sina noma mie - I have no objection.
Neno lingine ambalo watu hulichukulia kama la mtaani ni Nomi! .... (nyomi)
Tatizo lililotokea hapa ni kuwa watumiaji wanakosea badala ya kusema Nomi baadhi wanasema Nyomi! Mfano utakuta mtu anapiga stori alafu anasema 'katika mkutano hou watu walikuwa Nyomi (Nomi)
Katika Kamusi ya TUKI wameeleza maana ya neno NOMI
nomi kl in abundance: Machungwa yamejaa NOMI ----- oranges are in abundance.
.