Nina ex-wife ambaye kwa mda mrefu mawasiliano yetu tunafanya kwa ajili ya mtoto wetu mpendwa ambaye anaishi nae yeye. Zaidi ya hapo akinipijia labda kwa shari tu ila hatuna mawasiliano zaidi ya hapo. Sasa jana kanipijia simu tena alikuwa mpole hadi nikashangaa alichoniambia kuwa alitaka kunisalimia tu nikamshukuru nikakata sim, nikawa nawaza manake haijawahi kutokea mara akapijia tena akanambia this week anaomba tuonane nikamwambia ntachek kama nitapata nafasi. Kwa sasa nina wife wangu mwingine mpendwa naishi nae. Sasa ushauri kutoka kwenu maanake ninajiuliza sana hasa nini anachoniitia ni heri au shari nisaidieni