nisaidieni maana ya neno hili hata kwa maana ya lugha ya kingereza

nisaidieni maana ya neno hili hata kwa maana ya lugha ya kingereza

Van persie

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,099
Reaction score
720
"kibalakala" nimetafuta kwenye kamusi zote nimekosa,mwenye msaada tafadhali.
 
"kibalakala" nimetafuta kwenye kamusi zote nimekosa,mwenye msaada tafadhali.

Kuna njia nyingi za kujua maana ya neno mojawapo ni kuangalia jinsi neno lilivyotumika/limetumika wapi.Ningependa kujua wewe neno hilo umelipata likiwa limetumikaje au kama unaweza andika sentensi inayotumia neno hilo au wewe ulivyoiona imeandikwa au ulivyosikia.Ukiweza kufanya hivyo ni rahisi watu kukusaidia kuliko ukiomba neno kama lilivyo.
 
KIBALAKA au KIBARAKA ??

KIBARAKA ni yule mtu aliechaguliwa / aliepewa mamlaka na kuwaendea kinyume watu wake / waliomuweka / waliomchagua kwa kufata matakwa ya watu wengine.
KIBARAKA=KIKARAGOSI ambapo hucheza ( sio kwa amri yake ) kwa amri ya mchezeshaji. Hutumika sana kwa kusema viongozi wa nchi.
Wajuzi watakuja kukufahamisha zaidi
 
hili neno nilimsikia prof.kabudi alipohojiwa na jenerali ulimwengu,alilitumia katika muktadha wa kisiasa mfano wa sentensi"Kielelezo cha ufukara na sera za kibalakala nchini"
 
Kama bado unatafuta maana ya "Kibalakala" (Kibarakala):

"Barakala"=sycophant,flatterer,fawner
 
Back
Top Bottom