Nisaidieni makisio ya gharama ya nyumba hii

Forrest Gump

JF-Expert Member
Joined
Jul 2, 2021
Posts
637
Reaction score
1,532
Msaada tafadhari.

Nyumba ambayo bati haiendi juu sana. Kimo ambacho ni normal na standard
 
Wanasemaga 1ya 3 ya upana kwa mtindo wa kiingereza nyumba si ndefu
 
raughly kwa assumption maana Ramani haipo, hatujui mifereji ikataaje, aina ya muezeko, jinsi bati zitakatwa andaa bati pc 150-170 za futi 10 kwa 3
Kila lakheri
 
Size: 12m x 8m

Vyumba: Master room, bedroom, dining roon na living room.

Uzio: 20m x 20m.

Bati: Isio ndefu kwenda, gauge 28 migongo mipana.

Finishing: isio ya gharama sana na isio below average, urembo wa nguzo fensini, madirishani na barazani.

Eneo: Mara, kanda ya ziwa.

Nisaidieni kujua naweza kutumia bei gani kwa hadi kumaliza.
 
Ujenzi huu wa kisasa unapelekea kutumia bati nyingi sana.

Ni njia gani nzuri ya kupelekea uwezekano wa kutumua bati chache ila isiwe hidden roof house.
 
Nenda hospital yoyote ya wilaya utaona jinsi wanavojenga kwa kubana bati
 
Ujenzi huu wa kisasa unapelekea kutumia bati nyingi sana.

Ni njia gani nzuri ya kupelekea uwezekano wa kutumua bati chache ila isiwe hidden roof house.
Huna hela tu, hakuna ujenzi unao tumia bati nyingi ,we jenga mgongo wa tembo tu usijisumbue kushindana na waramba asali
 
Piga paa la kubwa jinga style

Yaani mbao zikaribie kulala kabisa
I nakosa show na JOTO unakuwa umeliarika rasmi ndani kwa sisi tunaoishi kwenye joto
 
I nakosa show na JOTO unakuwa umeliarika rasmi ndani kwa sisi tunaoishi kwenye joto
Kwanza mtaa utakao Jenga wote watakuwa wanakutolea mfano wa Nyumba yako.

Pili haitovutia kimuonekano hasa likiwa jumba kubwa.

Ukipiga JANGWANI style a.k.a Contemporary au Sina Hela mie ujue itavuja tu na kuongeza mzigo kwenye finishing.

Kifupi nakushauri tu, ukimaliza kozi tatu jipange taratibu uzuri Nyumba ya tofari haiozi.

Uje kupaua kwa Walamba asali style ambayo Nyumba itapendeza, kuwa makini na mabati feki, huwa inakera zikipauka wakati pesa umeitafuta kwa kung'ata meno.

NB: Nilikaa two years ndio nikaenda kupaua na kuweka grill, kumbuka ukiweka Nyeupe unajikuta upo peke yako kwenye huo mtaa.
 
Hahaahahahahahaha
 
Ujenzi huu wa kisasa unapelekea kutumia bati nyingi sana.

Ni njia gani nzuri ya kupelekea uwezekano wa kutumua bati chache ila isiwe hidden roof house.
Factors zinazopelekea idadi ya bati kuwa chache au kuwa nyingi

1. Design ya nyumba yenyewe, paa huwa linafata kona za kuta hivyo ni muhimu kuangalia design ya nyumba yako ilivyo kabla hujaanza ujenzi..kadri nyumba inavyokuwa na kona kona nyingi basi ndivyo paa linazidi kuwa more complex na kufanya wastage kuwa kubwa zaidi

2. Angle ya paa, nyumba inaweza ikawa moja lakini atakayepaua kwa kutumia angle 30 atatumia bati chache kuliko atakayepaua kwa kutumia angle ya 45 etc. Kadri angle ya paa inavyozidi kuwa kubwa ndivyo idadi ya bati huongezeka zaidi mfano ule mtindo wa bati za kuficha huwa wanatumia angle kuanzia 8 mpaka 15 ndio mana bati zinazotumika ni chache zaidi kuliko mifumo ya bati la kuonekana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…