Nisaidieni mawazo Wana JF

Retired

JF-Expert Member
Joined
Jul 22, 2016
Posts
44,629
Reaction score
83,056
Kuna mtu mimea/mazao yake imeliwa na mifugo wa jirani yake. Na Jamaa mwenye mifugo anakataa kuwa mifugo wake hawajaingia Kwenye shamba lake.

Utajengaje ushahidi kuwa kweli ni mifugo yake ndiyo imekula mazao yako na hali hukuikuta mifugo yake shambani mwako, ukaikamata kama kizibiti (exhibit).

Sheria unasemaje katika scenario kama hiyo?
 
Sababu zinazowafanya muamini mifugo yake imekula mazao ndio mzitumie kama ushahidi.
Waliambiwa tu na waliiona mifugo ile.

Nakumbuka zamani ukikuta mifugo Kwenye shamba lako unaikamata na kuitunza mpaka mwenyewe aje muelewane. Sasa hawakuwepo kuikamata. Unafanyaje?
 
Kama ni yeye pekee ana mifugo maeneo hayo kazi inakuwa rahisi sana. Tatizo ukute majirani wengine pia wana mifugo
 
Waliambiwa tu na waliiona mifugo ile.

Nakumbuka zamani ukikuta mifugo Kwenye shamba lako unaikamata na kuitunza mpaka mwenyewe aje muelewane. Sasa hawakuwepo kuikamata. Unafanyaje?
Labda ushahidi wa kimazingira au watu walioshuhudia tukio. Nao hawakupiga hata picha/video. Wafugaji wanakera sana
 
Hapo upelelezi wa kina unahitajika
Malisho ya mifugo yake ni wapi
Routine ya kulisha ikoje
Nyayo za mifugo nknk
 
Kama hakuna ushahidi hatalipwa, Cha kufanya alipe kisasi kama anaweza, maana Kuna makosa ambayo mtu hufanya, na ukakosa ushahidi lakini ni kweli kafanya, amfanyie kitu inaitwa Torati ili akome
 
Labda ushahidi wa kimazingira au watu walioshuhudia tukio. Nao hawakupiga hata picha/video. Wafugaji wanakera sana
Hakuna picha walizonazo. Lakini na picha wakizitoa si wenye mifugo wanaweza kusema this is an afterthought kuwa ni dramatized after the incident.
 
Hapo upelelezi wa kina unahitajika
Malisho ya mifugo yake ni wapi
Routine ya kulisha ikoje
Nyayo za mifugo nknk
Unfortunately Baada ya kula mazao ya jirani mvua ilinyesha na hivyo nyayo hazipo na Leo ni siku ya 14 wanatafakari wafanyeje maana uharibifu ulikuwa mkubwa, wameumia sana
 
Unfortunately Baada ya kula mazao ya jirani mvua ilinyesha na hivyo nyayo hazipo na Leo ni siku ya 14 wanatafakari wafanyeje maana uharibifu ulikuwa mkubwa, wameumia sana
Kwa Tanzania hapo ni ngumu maana zimeshapita wiki 2
 
Unfortunately Baada ya kula mazao ya jirani mvua ilinyesha na hivyo nyayo hazipo na Leo ni siku ya 14 wanatafakari wafanyeje maana uharibifu ulikuwa mkubwa, wameumia sana
Kama kuna watu walio ona tukio basi hili ni lakupeleka kwenye ofisi ya Kata/Kijiji/ ili huyo muhusika aitwe na awajibishwe. Hili shauri litasikilizwa hata kama tukio lilitokea wiki 2 zilizo pita, hapo hoja inaweza ikawa mlikua mnajaribu kufanya usuluhishi kabla ya kufikisha shauri kwenye ofisi ya mwenyekiti wa kijiji ama mtendaji wa kata.
 
Jirani anae haribu mazao yako kwa kutokua muangalifu wa mifugo yake, huyo hana adabu na anadharau kubwa. Hafai hata kudumisha nae ujirani.
Kuna kipindi usipotoa adhabu yenye kudhihirika unakuwa umetoa adhabu kubwa zaidi.Anajua kwamba unajua amekukosea halafu umemuacha.Ni adhabu zaidi ya adhabu.
 
asante sana
 
Ukikuta mfugo shambani chinja weka nyama kwa Friji ,Pasaka iko karibu mulaaa😅
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…