Nisaidieni na hili neno ttafadhalini

Nisaidieni na hili neno ttafadhalini

amani91

Member
Joined
Jul 21, 2012
Posts
41
Reaction score
6
maana halisi ya neno MWANAUME.

Sababu jana katika kijiwe fulani cha kahawa hapa mtaani kwetu karibia watu watoane macho.
:confused3:
 
Ni mwanadamu mwenye jinsi ya kiume! Labda tueleze mlichokuwa mnabishania ni nini!!
 
kwa kifupi Jamaa wanasema mwanaume ni mwenye familia na anajitegemea
 
kwa kifupi Jamaa wanasema mwanaume ni mwenye familia na anajitegemea

Hakuna kitu kama hicho sababu kama ndo hivyo basi hata msichana aliyevunja ungo na ana watoto nae ataitwa MWANAUME sababu atakuwa anaitwa mwenye familia na anayejitegemea
 
Hakuna kitu kama hicho sababu kama ndo hivyo basi hata msichana aliyevunja ungo na ana watoto nae ataitwa MWANAUME sababu atakuwa anaitwa mwenye familia na anayejitegemea

kuna mvulana na mwanaume, pia msichana na mwanamke..kijinsia wako sawa kwenye hayo makundi ila kuna utofauti wa madaraja ya maisha na majukumu katika familia!

Kwa muktadha huo hicho kilinge kilichokuwa na huo mkanasha walikuwa sawa kabisa!
 
neno mwana lina asili ya kibantu maana yake ni mtoto, mwanamume ni mtoto wa yeyote mwenye jinsia ya kiume. mwanaume ni nomino kuu, kiumri wanaume ndo jina tunalitofautisha tena inategemea na mazingira. mf.. nyumbani wote wenye jinsia ya kiume tunaitwa wanaume. maeneo yenye watoto wa rika fulani mf (15-22), nazungumzia shuleni na ktk nyumba za ibada watu hawa wanaweza kuitwa wavulana.....ni hayo tu ila wanaosema mwanaume ni mwenye familia wanakosea ni sawa na anaemuita mwanaume mwenye nguvu rijali na kusahau kuwa rijali ni neno la kiarabu linalomaanisha mwanaume
 
U sahihi kwenye tafasiri ya mwanaume....hapo kwenye al-rijal...pitia tena utapata maana halisi!
 
Limetokana na UUME (ub**), neno mwana nalo ni mtoto.
Hivyo itakuwa ni: mtoto mwenye ub** (mtoto wa kiume).

Pengine katika kukua na kuendelea kwa lugha ikasababisha kutumika hata kwa mtu mzima.

*mwanamke limetokana na uke (k***) na mwana ni mtoto hivyo tunapata maana ya:
mtoto mwenye k***.
 
kwa mm nijuaavyo mwanaume ni binadamu mwenye uume ila awe kesha balehee kama hajablehe anajulikana kwajina mvulana na mwanamke ni binadamu ambaye kesha vunja ungo kama hajavunja huyo ni msichana japo wengi huxema mwanamke ni ambaye ameshazaa au kuzalishwa sasa huko mm cpo naomba niwasilishe
 
nimewapata lakini nasubiria mtu mwenye uhakika kamili wanajamvi
:embarrassed1:
 
kwa mm nijuaavyo mwanaume ni binadamu mwenye uume ila awe kesha balehee kama hajablehe anajulikana kwajina mvulana na mwanamke ni binadamu ambaye kesha vunja ungo kama hajavunja huyo ni msichana japo wengi huxema mwanamke ni ambaye ameshazaa au kuzalishwa sasa huko mm cpo naomba niwasilishe
Hapana shaka yoyote kuwa ulivyosema ndivyo linavyotumika kimatumizi.

Ila ukiligawanya neno lenyewe MWANA na UME/MME utaona waziwazi kabisa hili neno limetokea kwa mtoto, ilikuwaje mpaka likafikia kutumika kwa binadamu mwenye uume kisha iwe aliyebalehe (kama ulivyoweka)? ..hapa ningependa kusikia watafiti wanasema nini.
 
jamani unajua neno mwanaume lina maana nyingi na kila mtu anatoa maana yake kwa mf. mm naweza sema mwanaume ni yule anaye jituma kwa vyovyote vile pia akisikia neno mwanaume asifiwi kula bali mwanaume anasifiwa kazi nihayo tu.
 
Kwa mujibu wa kamusi ya kiwahili sanifu (2004) neno Mwanamume/mwanaume lina maana ya mtu yeyote mwenye jinsia ya kiume.
 
Nadhani wakati mwingine neno "Mwanaume" linaweza kutumika kama Kielezi. Kuelezea hali'Jambo ka kiume. Mfano, hata binadamu mwenye jinsia ya Kike anaweza akaitwa mwanaume.
Hujawahi sikia mwanamke anaambia "Kweli wewe ni mwanaume". husasani baada ya kufanya jambo ambalo linaonekana nia kubwa au gumu.
 
Nomino mwanaume limeundwa kwa kuunganisha nomino mbili tofauti MWANA pamoja na UME, hivyo neno MWANA linamaana ya MTOTO na UME limetokana na UUME (ubo**) hivyo MWANAUME linamaana ya MTOTO mwenye UUME haijalishi rika bali kinachaangaliwa ni UUME. Mwanamke akifanya kazi nzito huambiwa we ni mwanaume kweli, hiyo isikuchanganye kwani hizo ni sifa tu na hazibadilishi yeye jinsia cha msingi ni kuangalia mtt ana uume, ninapozunguzia MTOTO simaani mtoto mdogo hata mtu mkubwa ni mtoto kwa wazazi wake. nadhani umenielewa aksante kwa kuuliza swali lako kwani "kuuliza si ujinga" na "asiye uliza hana ajifunzalo"
 
Kiswahili chetu cha unguja mjini mwanamme ni mwenye jinsia ya kiume na mwanamke ni mwenye jinsia ya kike.
Hayo ya mvulana na msichana nayaskia huko bara.
Ni kama kwenye English girl/woman na boy/man wametafautisha according na age pamoja na hayo mambo ya majukumu
 
Back
Top Bottom