Achana nae mjomba, mwambie huo ndio msimamo wako, kama unampenda mpenzi wako kwa dhati
mjomba nae, kuishi na wewe anataka hadi akuchagulie mume, usikute keshakula pesa za watu
kuna wasichana waliharibiwa maisha yao ya kimahusiano na ndugu kama hao, na mpaka leo wameshikilia
mchuma siti ya kukaa hakuna
Nikwambie mrembo, wakati nataka kuolewa, nilikatazwa na kila mtu, kwangu mie nahisi ilikuwa kwa nia nzuri tu
sababu nilikuwa mdogo, yaani ndio kwanza nimemaliza form 4 tu, watu walikuja juu sana, itakuwaje uolewe, mara mtoto
wetu anajitahidi ila unamkatiza shule, nusu niwasikize, ila moyoni nilijua kabisa huyu ndie mume, nikashikilia msimamo
niliolewa na mengine yote waliyotaka nifanye nikayafanya ndoani, kwa hiyo kama unahisi toka moyoni ndio huyo jamaa unampenda olewa
ili hata kama mambo yakienda mrama usijute huko mbele,mwambie mjomba huyo ndiye mume uliyechaguliwa na Mungu
Pia sali Mungu akuonyeshe njia sahihi