Nisaidieni namna ya kuepuka rushwa kazini

kavulata

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2012
Posts
13,778
Reaction score
14,214
Nina watoto 3 ninawalea bila baba yao, Nakaa yumba ya kupanga Tandale kwa Tumbo Nafanyakazi ya uuguzi hospitali moja kinondoni, baada ya makato yote mshahara wangu ni sh. 547,058.24. nauli yangu sh. 1300 kila siku, mtoto mkubwa yuko form 2 shule ya King'ong'o kule Ubungo, wa pili yuko la 5 na wa 3 yuko 2. Kazi yangu inahitaji kuwa msafi, upendo, kuongea, kuchekea wagonjwa na wateja wengine, kuwahi kazini na kuvaa uniform nadhifu. Lazima niwe na afya nzuri ili kumudu kuwahudumia wagonjwa vema pamoja na kujikinga dhidi ya magonjwa ya kuambukiza kutoka kwa wagonjwa. Ikifika tarehe 17 pesa imekatika na kunifanya nikose furaha nyumbani na kazini, nawaza namna nitakavyomudu ku-smile kwa upendo kwa wagonjwa wangu kutokana na mawazo ya kukosa nauli, chakula na mahitaji mengine kiasi cha kutamani kuomba rushwa japo nipate nauli na chakula. Naomba kwa wenzangu ambao na wao wanasema hawana. Wakati mwingine najihisi kuwa labda nina matumizi ya hovyo yanayosababisha niishiwe hela mapema kabla ya wakati. ndio maana nikaandika uzi huu ili mnichangie mawazo kama kuna mwenye utaalamu wa kuweza kuzipangia sh. 547058.24 katika kutumia ili niepuke na kutamani mchango kutoka kwa wagonjwa au vitendo visivyompendeza mungu na jamii. kama kuna mchumi au mtaalamu anipanue mawazo.
 
Hapo upende usipende hakuna kitakachobalance....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…