kuna mtu kakujibu kwamba anamfahamu muuzaji wa vifaa vya ujenzi ambaye anakukopesha vifaa vyote hadi unamaliza. Huyu aweza kuwa mzuri kuliko benki. Sijui atakutoza riba kiasi gani lakini mimi kwa uelewa wangu aweza kuwa mzuri zaidi ikiwa vifaa vyake ni vya viwango.
Hapa Tanzania, benki karibu zote zinatoa commercial loans tu. Yaani mikopo kwa ajili ya watu wanao nunua bidhaa na kuuza. Unapewa mkopo mwezi huu, mwezi ujao unaanza kulipa. Wakikupa grace period, basi utakuwa unalipia riba kwa kipindi chote cha grace period. Grace period ikiisha unaanza rasmi kulipa mkopo wako, hivyo riba uliyokuwa ukilipa kipindi chote (grace period ) hiyo ni kachumbari ya benki kwani haipunguzi deni lako hata senti.
Pili kama utasema ukapime kiwanja chako, bado mabenki yatakuambia kwamba hawakopeshi mteja mwenye plain land. Wao wanataka pawe na nyumba.
Benki ya Tanzania Women Bank ilikuwa ikipokea hati za makazi lakini nadhani wamesha badili japo sina uhakika. Lakini nayo wewe bado uwezi pata maana hapana nyumba.
Hitaji lako ni genuine lakini taasisi zetu za fedha zipo hivyo. Jaribu fuatilia huyo mwenye kukopesha hardware lakini kwa kuwa dunia ya leo imebadirika basi nako uende kwa tahadhari kubwa na mkiingia mkataba uwe na mashahidi wenye uelewa na wanaopenda maendeleo yako.
Naomba kuwakilisha