Nisaidieni nifanye biashara gani? Nina mtaji wa 3,000,000/=, nipo Himo-Moshi

usikimbilie kufanya biashara yoyote kisa una mtaji hakikisha unaelimu yakutosha juu ya hiyo elimu kwanza kisha uwanze kuifanya.
 
Mkuu mie sikubaliani na wewe unapotaka mwenye idea kukaa physically kwenye biashara coz mtu huyu anaweza kuwa na miradi mingi na cha muhimu kwake ni kuhakikisha anakagua na kuhakikisha waendeshaji wanafuatilia vision yake kama jinsi alivyoplan mwanzo. Otherwise wewe unaongelea yule kijana anayefanya kibandani pekee na mtazamo wako si kwa mfanyabiashara mwenye multiportfolio investment/assets. Chukulia mfano una projects zaidi ya 3 at par moja iko Dar, Arusha na Mbeya utakaa wapi sasa? na je huoni kuna kampuni na wafanyabiashara wengi wamefungua branches na hawakai physically bt biashara wanafanya external supervision na zinafanya vizuri in terms of market and competition dhidi ya rivals?





 
Mwalimu bado upo Himo? njoo hapa Freedom nikuungishe kama ulishapata biashara ya kufanya
 
himo moshi napajua saana..
pale kwa capital yako sio ndogo kwa himo waweza fanya mengi kama ifuatavyo..
waweza nunua contena then upangishe..
waweza fungua duka la bidhaa za umeme coz watu weng wanajenga huko..
waweza anzisha restaurant nzur ya quality services hala himo mjin wateja wapo sana..
 
fanya biashara ya kufuga samaki,unahitaji nyumba yenye fensi, na kuchimba vidimbwi vya futi 3 ,vidimbwi kumi ,chakula cha samaki na kuwanunua samaki kadhaa,kwa maelezo zaidi tafuta kwenye google
 
acha kuwafanya watu hawana akili heshimu mawazo ya watu sio kujiona wew ndo unaakili, na kwa taarifa yako mawazo waliyotoa wachangiaji wengine yanafit mahali popote na mkoa wowote pia na hali ya hewa yoyote,hebu nibishie kama biashara ya kufuga samaki inachagua mazingira au ?
 

Una bishana na nani mkuu?
 
WAZO LANGU.
1.M-PESA/TIGO- PESA
2.NERT WORK MARKETING
3.DUKA LA VINYWAJI LA JUMLA
4.DUKA LA JUMLA BIDHAA MCHANGANYIKO.
HAPO VIPI.:car:

Kwa kuwa ni mwalimu nadhani network market itamfaa sana
 
Uza unga haukosi wateja.

Toa maelezo ya kutosha basi FF.!

Hii biashara kuna kampuni moja ndogo tu inaifanya na inaingiza pesa za maana sana!

Kwa mwezi naambiwa mwenye coy anachezea mil 300 kwa ku supply tonnage 15 za unga wa mahindi.

Biashara nzuri sana hii.
 
biaashara ya msimu hapo ni kununua nafaka, tia dawa, piga stoo. Kuna msimu Kenya bei inapanda sana, unauza huko
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…