Siku zote ndoa inayoendeshwa kwa uwazi wa mambo yanayowahusu wanandoa hujaa amani ya kutosha! Huwa sioni mantiki yoyote ya wanandoa kufichana mambo! Eti simu!,hivi mmeshawahi kujiuliza maisha ya wanandoa yangekuwa na amani kiasi gani kama matumizi ya simu yasingekuwepo?! Kwa nini tumeshindwa kuzitawala simu na badala yake zimetutawala?! Inasikitisha sana! Mi nadhani kila mwanandoa anapaswa kuwa wazi na sio masuala ya kuwekeana mipaka! TUACHANE NA MAISHA YA MAIGIZO JAMANI NA KUMBUKENI NDOA ZILIKUWEPO KABLA HATA YA HIZO SIMU KUVUMBULIWA!!