MASHIRI
New Member
- Mar 16, 2013
- 3
- 0
<strong>Jamani wadau wa sheria naombeni msaada!<br>Mi nimekua mfanyakazi wa kuajiliwa shirika fulani hapa TANZANIA yapata miaka 8 lakini nimeamua kuacha kazi mwezi ulioisha ili niendelee na maisha mengine. katika mwezi wote huo nimejaribu kufuatilia barua ya kuacha kazi nimekua nikizungushwa kwa madai ya kwamba nimeacha kazi kati kati ya mwezi kwahiyo nimeipa hasara kampuni, sikufahamu kama sheria inasemaje juu la swala la kuacha kazi ni lazima iwe mwisho wa mwezi au la!nilipambana nikapewa barua lakini sasa kuna lingine ambalo ni zito sana kwangu. Ndugu msomaji nimeenda kupeleka barua yangu NSSF nikaangalia na mafao yangu nimekuta MWAJIRI wangu ameweka 20% ya fedha zangu kwa miaka yote nane. Naombeni msaada wenu nifanyeje maana NSSF wameniambia tarehe 04/06/2013 niendee check yangu ya hiyo 20%. Naombeni msaada wenu wadau mnisaidie nipate mafao yangu yote 100%.<br> Naomba sana msaada wenu ni harakati za ukombozi kjwangu na kwa wengine wenye matatizo kama yangu.<br></strong>