Pole BLISS...ujauzito wako wa wiki 28 si sababu ya wewe kujaa gesi tumboni. Tumbo la uzazi na chakula ni tofauti na hayaingiliani kabisa. Inaweza tu ikawa sababu ya chakula ulichokula. Kama ni tatizo la mara kwa mara na linafuatana na maumivu ya tumbo hasa maeneo ya chembe, basi muone daktari inaweza ikawa gastritis ambayo inaweza ikakuletea ulcers baadae...lakini kama ni leo tu, au mara moja moja...unaweza ukatumia Andrews ile unachanganya na glass ya maji safi unakunywa. Haina athari kwa ujauzito wako.