Nisaidieni Usaha unatoka kwenye fizi mtoto wa miaka 5

Nisaidieni Usaha unatoka kwenye fizi mtoto wa miaka 5

Machuchu

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2017
Posts
1,260
Reaction score
965
Za leo ndugu zangu.
Mwanangu alikuwa anasumbuliwa na jino ambalo ni gego, jino ili halimuumi mara kwa mara anaweza kukaa mwezi au miezi 2 halimuumi then linakuja kumuuma.

Cha kushangaza wiki iliyopita kama mungu nimemwambia fumbua mdomo niangalie jino nakuta kwa pembeni kwenye ufizi pamevimba sehemu ya jino linapo muuma ni gego la mwisho chini.

Nikamgusa akasema anaumia ila anakula mswaki anapiga bila shida nikampigia rafiki yangu ni nesi temeke nikamwambia akasema mnunulie Cloxaylline au Amoxylline ila nikampa iyo dawa ya kwanza pia akasema awe anapigia Sensodyne mswaki.

Niliambiwa itamsaidia iyo dawa ila toka nimempa sasa ni wiki na leo asubuhu nimejaribu kumuangali bado pamejaa nikajaribu kupagusa ameruka na usaha ukatoka tena.

Ijumaa anamaliza dawa nataka nimepeke Temeke Hosp kwa dokta jumamosi, Je, nani alishawahi patwa na tatizo ili dawa gani ilimsaidia.
 
Asante, ila muhimbili pale mimi mgeni sijui ata naanzia wapi na gharama zake kama unajua please nipe mwongozo japo kidogo.
Kuna kitengo cha meno na wana clinic ya watoto pia unaweza kuuliza utaratibu wa kuonwa wanafunzi chini ya usimamizi wa mwalimu wao, huduma hii hulipii kwani dental students wanajifunza practical kwenye tatizo lako.
 
Ilo jino lime pekechwa..!? Au lime haribika..!?
Mahali penye pus( usaa) panakuwa pana secondary bacteria infection. Fanya utafute syp: cephalexin 7.5 mls 1x3. Apate na hydrogen peroxide mouth wash hizi zita msaidia kupunguza infection. Ila kumuona Dr wa meno ni muhimu kama ulivyo shauriwa na SKY ECLAT
 
Sawa nitapita kesho nikaulize utaratibu unakuwaje then nimpeleke
 
Pole sana usiwaze hilo tatizo linatibika...cha msingi fuata ushauri wa wataalamu hapo juu mwanao atapona tu
 
Ilo jino lime pekechwa..!? Au lime haribika..!?
Mahali penye pus( usaa) panakuwa pana secondary bacteria infection. Fanya utafute syp: cephalexin 7.5 mls 1x3. Apate na hydrogen peroxide mouth wash hizi zita msaidia kupunguza infection. Ila kumuona Dr wa meno ni muhimu kama ulivyo shauriwa na SKY ECLAT
Hapana halijapekechwa wala kuoza limecrake kidogo tu
 
Hapana halijapekechwa wala kuoza limecrake kidogo tu
Ok. Fata ushauri nilio kupa. Alafu nenda agha khan pale wata kwenda iziba iyo crack jino litakuwa vzr..
NOTE: mda unavyo zidi kwenda ndo tatizo huwa linazd kukua na laweza sababisha jino kung'olewa.
 
Muone dentist mkuu mpeleke Muhimbili
Nimeenda leo wamekataa kunihudumia wamesema hadi barua ya Transfer kutoka temeke, wamesema huduma ya moja kwa moja huwa ni wagonjw wa emergency. Kesho nitaamkia temeke mapema tu. Asante sana mungu akubariki
 
Nunua hydrogen peroxide mouth wash asukukutue na mswaki kila baada ya masaa nane kwa siku Saba .then utaona mabadiliko
 
Back
Top Bottom