Nisaidieni Wana JF-nataka kutoka

engmtolera

JF-Expert Member
Joined
Oct 21, 2010
Posts
5,149
Reaction score
1,441
Wana JF

Mimi kijana mwenzenu ninayetegemea kujiondoa ktk maswala ya kuajiliwa na nataka kujiajiri mwenyewe

ktk kufanya hilo nime amuwa kuanzisha kampuni yangu binafsi nitakayo isimamia mimi mwenyewe.


Wana JF Nawaomba msaada tena msaada huu utanitowa hapa nilipo na kunipeleka hapo ninapokusudia

Nategemea kuanzisha kampuni itakayojishughulisha na uuzaji na usambazaji wa vifaa vyote vinavyo husu maswala ya SOLAR POWER hapa kwetu Tanzania

Naomba msaada wa kumpata mwanasheria atakaye nisaidia ktk kuisajiri kampuni yangu,sina maarifa yeyote na mambo ya sheria juu ya uanzishwaji wa kampuni binafsi,sijui nini kinahitajika na wapi

kama yupo mtoa msaada basi tushikane mikono na kuinuana ktk hili


Kampuni yangu itajulikana kwa jina la IHAM SOLAR SUPPLIERS office zitakuwa Morogoro kwa kuanzia




Karibuni kwa mawazo,kwa pamoja tutafika

SOLAR POWER FOR LIFE-PIA SOLAR POWER NI RAFIKI WA MAZINGIRA
 
hongera sana kwa kupania KUTOKA kama alivyoshauri rais wetu kwa viongozi.
kwa kuanzia, usimwage kuku kwenye mchele wako kidogo,watakufilisi. sio vizuri kumwaga details zote hadharani,hapa inawezekana mtu akawahi na kufanya vyote unavyofikiria kabla yako (formula ya syrup ya coca cola hata meneja mkuu haijui,analetewa kwenye kidumu tu). sidhani kama kwa kuanzia unahitaji mwanasheria,nadhani ungeweza kusajili kampuni kwanza halafu ukaona usiyoweza kufanya mwenyewe ndo utafute msaada. jaribu kufika brela kwanza uone watakuambia nini. kila la heri, wazo zuri sana na mie nakuwa mteja wako
 

thanks ,wazo nimelichuwa na nalifanyia kazi
 
kwanza hongera sana na mungu akuongoze kwenye malengo yako mazuri, uko sahihi, kwa sasa ni muhimu sana kumtafuta mwanasheria au mtu professional anayejua mambo ya kwanza ya kujisajiri na maswala mazima ya kulipa kodi na cost nyingine muhimu, i hope utatoka tu wangu
 

pamoja mkuu,namsubiri huyo atakaye jitolea kunitoa ktk hili wimbi,pia nami naendelea kuwasiliana na brela nijui nini cha kufanya
 
pamoja mkuu,namsubiri huyo atakaye jitolea kunitoa ktk hili wimbi,pia nami naendelea kuwasiliana na brela nijui nini cha kufanya

Brela muhimu, ila angalia wale jamaa siku hizi hawaeleweki, unaweza ukajiandikisha then ukajasikia faili lako limepote mikononi mwao
 
Wazo zuri sana ndugu!

Wasomi wetu wengiine nao wangekuwa na mawazo ya kuanzisha vitu kama hivyo ingesaidia kupanua ajira kwa wa-TZ wengi. Lakini sasa hivi unakuta wasomi ndo wanabanana mijini kutafuta ajira hawana mawazo ya kujiajiri.

Na wengi wa wasomi wetu ni waoga wa kukabiri changamoto!!

Nashindwa kuelewa mitaala ya vyuo vyetu inaandaa watalaam gani hasa? Hivyo ndugu komaa na hilo wazo lako wala usiachie njiani, hiyo ndo itakayokutoa!

Nami niko njiani kuchomoka kwenye hizi ajira za watu nikasaidie wengine kupata ajira, maana naona huku kama nanyonywa tu!!
 
 
Mkuu wazo ni zuri; Lakini nilifikiri utasema unataka kuanzisha kampuni ya utengenezaji wa vifaa vya solar, kumbe unaanzisha kampuni ya kusambaza vifaa. SWALI; Je utavitoa wapi?. Sasa umefika wakati wa kubadili mitazamo yetu badala ya kukimbilia kuwa WAHUUZI au WAMACHINGA ni vyema kufikiria kuzalisha bidhaa, hivi biashara za uchuuzi haziwezi kututoa kwa haraka. Hivyo basi mimi ningekushauri ufikirie mbali zaidi ya hapo.
 
Reactions: LAT

Ni kweli mkuu, Wa Tanzania wengi ni Wafanya biashara na si Wajasiriamali.
 
 
Ni kweli mkuu, Wa Tanzania wengi ni Wafanya biashara na si Wajasiriamali.

na hilo ndio tatizo letu watanzania wengi...ujasiriamali ni tofauti kbsaaa na ufanya-biashara za kichuuzi.... kaka anataka kuwa supplies agent na sio mjasiriamali..full stop
 

Nikutoe wasiwasi juu ya hilo ulilonalo
kwani hilo ulilo liongelea nina mtazamo nalo ila kwa sasa bado kipato changu kinaniruhusu kuanza na hili na baada ya hapo mungu akibariki biashara basi naweza kulifikilia hilo

kuhusu wapi nitapata hivi navyo taka kuvifungulia kampuni hii si tatizo,tayari mimi ni member wa baadhi ya viwanda vinavyotengeza vifaa vyote vinavyohusiana na solar ni swala la mimi kukamilisha hii kampuni na kuanza kazi

namshukuru mungu kuwa nina hata kaujuzi ka kutengeneza solar panel mwenyewe ili mradi tu niwe na solar cells,na pia nina uwezo wa kudesign solar system ya aina yeyote ile cha muhimu ni nafasi na maamuzi,hii ni elimu niliyo ipata pale sokoine university wakati nasoma degree yangu ya kwanza ktk maswala ya Agricultural Engineering

pamoja daima
 
na hilo ndio tatizo letu watanzania wengi...ujasiriamali ni tofauti kbsaaa na ufanya-biashara za kichuuzi.... kaka anataka kuwa supplies agent na sio mjasiriamali..full stop

lakini hata mazingira yenyewe yanaturuhusu kuwa hivyo, kwa mfano mimi naweza kutengeneza Home solar panel lakini ni local made,yaani ni ya kutumia kopa materials kiasi kwamba hii itanichukuwa mda mrefu sana kufika malengo,ila baada ya kukamilisha na mambo kwenda vyema basi chochote cha weza kutokea ili mradi tu VIKWAZO na WALAJI wasikwamishe kile ninachokifikilia
 

ni me ku pm mkuu
 
Hongera sana kijana kwa kutaka kujiajiri ila kunasiku ulituanzishia thread hapa kuwa hiyo kampuni ipo tayari na inafanya kazi au ulikuwa unajaribu soko nini mzee? I wish you all the best
 
Hongera sana kijana kwa kutaka kujiajiri ila kunasiku ulituanzishia thread hapa kuwa hiyo kampuni ipo tayari na inafanya kazi au ulikuwa unajaribu soko nini mzee? I wish you all the best

haikuwa kampuni,ila nilikuwa nazitangaza baadhi ya solar panel kwa bei nafuu,ila kwa sasa nimesha zimaliza ziligombaniwa sana

lakini sasa nimekuja na ujio mpya ni lengo la mda mrefu na sasa nalipeleka mbioni

kwa kweli nawashukuru sana wadau kwa michango yenu,

kama muonavyo umeme unazidi kuwa ni Tatizo,kwa hiyo solar power ni kila kitu

ingia hapa Welcome to the IHAM Solar Suppliers
 
Nipe Price ya Solar Panel inayoweza kuendesha pump ya kisima cha maji nataka kuchimba kisima shamba ambapo hakuna umeme muhimu sana mkuu nitumie
 
Hii kampun yako mbona yaonesha kama ipo hewani, mpaka umeanzisha na mawebsite tayari?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…