Haya mambo ya ngeli nimeshayasahau, ila kwa kwa kumbukumbu kidogo nadhani zipo dhana mbili kuhusu Ngeli.. Utaweza kujua tofauti ya vitu na watu (viumbe hai) kwa kuangalia mifano yangu inayofuata.
Kipofu, kiziwi, (kijana pia) - Amekula, anacheza, ameanguka -- watu (ngeli ya KI-A)
Kiti, kiberiti - kimeanguka, kimepotea--- vitu (ngeli ya KI-KI)
Vipofu, vijana - wanakula, wanacheza, wanaanguka --- (Ngeli ya VI - WA)
Viti, Viberiti - Vimeanguka, vimepotea (ngeli ya VI-VI)
Ukitazama utaona kuwa hata neno -kijana, vijana- linaingia katika kundi la vipofu na viziwi, naamini yapo maneno mengine ambayo yanaingia hapo pia..
Wataalamu wa lugha watafafanua zaidi.