Hii ilinitokea mimi, sister yupo shirika la umma mi nipo nipo tu sina mishe
Katika moja na mbili nikawa namwambia anipige tafu mdogo wake akawa ananiambia majukumu yake
Siku akaniambia anaenda kukopa milions kadhaa ili anunue gari, nikamwambia usinunue gari fungua kitega uchumi kiwe kinakuingizia pesa akanipuuza
Kanunua gari, kafanya na mambo kadhaa pesa imekata
Akabaki na deni kalipa deni kamaliza nikamwambia nikopee 3 mil kisha ntakuwa nakulipa kila mwezi au kama huniamini nifungulie ofisi nitakuorodheshea vitendea kazi ninavyovihitaji niwe napiga kazi jioni utakuwa unapitia hesabu kisha mimi utanifikiria, pia haikumuingia
Nikasema isiwe kesi mi mwanaume na nipo tayari kufa nikiwa natafuta kwa njia halali (kipindi hicho napiga mishe kiwandani nalipwa 169k kwa mwezi)
Nikakaza nikawa napiga overtime kwa mwezi nikawa naambulia 220k takehome
Huku kitaa kuna mwana (RIP) alinipa laptop baada ya kuona nipo fresh kwenye mambo ya IT, nikawazaaaa nikaona huu mshahara hapa kiwandani siwezi kutoboa zaidi ya kuishia kwenye kula na kulipa kodi ya chumba
Nikazama Dubai ya Dar kuulizia tool nakuta 325k, nikacheki AliExpress nakuta 180k nikajilipua kuagiza baada ya mwezi nikatumiwa sms na posta nikachukue mzigo wangu
Nikasema sasa tayari Laptop ninayo na Tool ya kuanzia maisha tayari ninayo, nini kifuatacho, ni kuacha kazi yes naachaje sasa?
Maana nikiandika barua ya kuacha kazi nitakosa stahiki zangu na PPF pia watanizingua
Nikasema ngoja niwazingue mabosi wanifikishe kwa HR ili wanitimue kazi ofcoz hili wazo likapita, nikawazinguaaaa mwisho wa aiku wakajaa mpaka kwenye vikao vya utovu wa nidhamu nikawa nawajibu shit
Wakaafikiana wanifukuze, hapo mimi siwazi maana nauamini uwezo wangu, pili nimeshapoteza 4 yrs sioni la maana nililifanya, nikasema ntajua mbele ya safari
Siku ya siku nikalimwa barua ya kuachishwa kazi then wakanipa kama 700k hivi nikasema fresh maana hata wasingenipa nilikuwa nna uhakika wa kutoboa maana nilishajipanga
Mtu mzima kiroho safi bila connection nikazama Dubai ya Dar kuanza kupambana
Nikapambana kama wiki mbili tu tabia yangu ya uaminifu na uwezo wangu katika kazi vikanifanya nipate goli
Kuanzia hapo mambo yakawa bam bam
Sa hivi mimi ndo nampiga tafu sister japo yeye bado yupo serikalini ila anakwamaga, maana anapokea mshahara wa digit 7 ila akishakatwa madeni anabaki na bajeti ya kula tu na hapo anasomesha watoto watatu
Kimoyo moyo najisemea wee ngoja siku ukinikalia vizuri nitakufundisha namna ya kutumia mikopo