Niseme jambo kuhusu Manara

Kwani Manara alimtukana tusi gani Mo na Barbara?
 
Nawaza akiamua kuwa msemaji kama shabiki kabla ya mechi nani atasikilizwa zaidi na mashabiki wa soka? Msemaji wa simba au shabiki manara?
 
Kwamba Mo hawezi kulilia umaarufu. Em aache kutukuza matajiri ajue nao hao ni binadam pia kuna upuuzi huwa wanaufanya.
Kwenye hilo manara anaweza kua sahihi.
 
Mashabiki wa Simba wanamuona Manara peke ake ndio tatizo na kweli ana matatizo lakini kwa upande mwingine boss kubwa ndio tatizo kubwa zaidi hilo ni suala muda tu
 
Mashabiki wa Simba wanamuona Manara peke ake ndio tatizo na kweli ana matatizo lakini kwa upande mwingine boss kubwa ndio tatizo kubwa zaidi hilo ni suala muda tu
Kila uto anapiga ramli kwa kusema eti 'ni suala la muda tu'. Kumbuka miaka minne ni muda mrefu, na wa tano unaingia!
 
Kila uto anapiga ramli kwa kusema eti 'ni suala la muda tu'. Kumbuka miaka minne ni muda mrefu, na wa tano unaingia!
Kwa maisha ya taasisi miaka minne ni kama masaa tu, Simba ipo ilikuwepo na itaendelea kuwepo ila watu wanaoingia na kutoka simba
 
Umaarufu upi anaolilia MO, kigezo gani kimetumika kusema manara kamzidi umaarufu MO?
Sijui mkuu hayo maswali muulize mo na manara wenyewe. Hapo mi nilichopinga ni hiyo kusema flani hawezi kitu flani. Isemee nafsi yako sio kumsemea mwingine ilhali nae ni binadamu.

Mo anapenda kupewa attention mzee hilo halina ubishi. Ndio maana nkasema yawezekana ni kweli pia.
 
Tajiri kijana sisi makombe tu
 
Hujui uliongeo ndg na umeandika pumba tu ukibase upande mmoja

Ungekuwa na akili ungechanganua ukiangalia makosa ya pande zote

Kunywa uju ulale[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Nawaza akiamua kuwa msemaji kama shabiki kabla ya mechi nani atasikilizwa zaidi na mashabiki wa soka? Msemaji wa simba au shabiki manara?
Hapo atakuwa anaendeleza ujinga alio nao yaani akatae kuwa msemaji kwa 700,000/= kwa mwezi halafu awe msemaji wa bure. Simba watafurahi sana.
 
Kwa jinsi Manara anavyoendelezaa bifu na Mo huko kwenye ukurasa wake Insta imenifanya nifikirie mara mbili mbili kama jamaa yupo vizuri "upstairs". Mbaya zaidi analeta mpaka ubaguzi kwa kukejeli asili ya Mo ambalo ni jambo baya sana kwani anataka kupanda mbegu ya chuki ambayo ikimea kila mtu mwenye akili timamu anajua matunda yake nini. Anasahau kuwa wakati yeye alipokuwa na mabifu na watu mbali mbali hasa watangazaji na waandishi wa habari walipofikia kumkejeli kuhusu hali yake alikuwa anaomba msaada kwa wakubwa wa nchi hii mpaka kwa "mwendazake".

Yaani huyu Manara nilianza kuwa na wasi wasi na "upstairs" yake wakati alipopata tatizo la macho. Wakati anaumwa macho watu mbali mbali walimchangia wakiwemo mashabiki wa Yanga zikapatikana pesa akaenda kutibiwa nje. Baada ya kupona akakaa baada ya muda akapata pesa basi kila akitaniwa na mashabiki wa Yanga yeye badala ya kujibu utani wa jadi yeye anabeba pesa eti anaenda makao makuu ya Yanga kuwarudishi pesa zao. Akasahau kabisa pesa aliyochangiwa wakati anaumwa na ana shida hata kama ilikuwa ndogo kiasi gani ilifanya kazi kubwa tofauti na pesa aliyotaka kurudisha kwa mashabiki wa Yanga. Yaani ni sawa sawa na mtoto anayetaka kuwalipa wazazi gharama zote za kumtunza akiwa mtoto mdogo baada ya kuwa mtu mzima na kupata pesa nyingi.

Ni kweli kila binadamu ana mapungufu yake hata Mo na Babra wana mapungufu yao kwa sababu sio malaika ila mapungufu ya Manara ni balaa kwa maendeleo ya Simba. Kitendo cha kuendeleza bifu mpaka sasa maana yake anataka Simba kama taasisi ifanye vibaya ili aonekane yeye ndiye alikuwa anasababisha ifanye vizuri. Na ukiangalia "post" zake hauhitajiki kuwa na akili za ziada kujua kuwa kama yangekuwa mapenzi yake basi hata leo ingewezekana angeisambaratisha Simba kabisa ili arudi akaichezeshe ndondo Meatu.

Eti Manara ndio mtu aliyekuwa anajifanya kuwa anaipenda Simba kuliko mtu yoyoyte yule mpaka akazamia mara tatu South Afrika wakati Simba anapigwa goli nne na Kaizer. Yaani huyo jamaa bonge la msanii Ray Kigosi akasome upya kazimia mara tatu halafu hakufa. Kiukweli kabisa mtu ambaye ni Simba damu ataipambania kufa na kupona "no matter" kagombana nani kwenye timu. Kimsingi sasa hivi Manara kadhihirisha wazi kutokana na matendo yake kuwa hata Usimba wake ni wa mashaka sana. Naanza kuwaamini watu wanaosema Manara ni Yanga pale Simba alifuata tu pesa na umaarufu.

Kazi kwenu bodi ya Simba kuilinda taasisi yenu kwani nyie ndiyo mliopewa dhamana na wanachama kuilinda. Nafikiri mtachukua tahadhari na hatua stahiki tena kwa wakati kuilinda taasisi yenu iendelee kuwa imara kuliko ilivyokuwa jana.
 
Hujui uliongeo ndg na umeandika pumba tu ukibase upande mmoja

Ungekuwa na akili ungechanganua ukiangalia makosa ya pande zote

Kunywa uju ulale[emoji23][emoji23][emoji23]
Anajua Manara Hana hela lazima aegemee upande wa ulaji wabongo tuko hivyo, eti naye no mchambuzi hpo hpo anadai Manara alikuwa akikimbia na michango ya mikoani, huoni ndo wale wale wachambuzi uchwara, can he prove that?

Sent from my 5033X_EEA using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…