Nishafuta namba yako

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,497
Reaction score
4,775
NISHAFUTA NAMBA YAKO

1)Natazama namba yako,simu haina thamani
Mi sipo moyoni mwako,namba yako sa ya nini
Nafata kauli yako,ulisema mdomoni
Sitaki upige tena,nishafuta namba yako.

2)Kumwacha umpendae,inaumiza moyoni
Pendo ulifurahie,liwaingie moyoni
Lazima ujioangie,mfikiri kwa makini
Sitaki upige tena,nishafuta,namba yako.

3)Penzi ni sawa na maji,uyatiapo kinywani
ukileta ujuaji,yatakukwama kooni
Uyayuke ka theluji,utoweke duniani
Sitaki upige tena,nishafuta namba yako.

4)Najua penzi si vita,vipi niwe mashakani
Japo roho ilisiota,ila leo burudani
Nambayo nimeifuta,baki na wako mwandani
Sitaki upige tena,nishafuta namba yako.

5)Hukuwa yangu bahati,kuwa nami maishani
Kupata penzi la dhati,kwanza muombe manani
Penzi ni kama kabati,fungua uone ndani
Sitaki upige tena,nishafuta namba yako.

6)Na usiku n ilalapo,sikwoni tena ndotoni
Nilipo wewe haupo,ni kweli siyo utani
Penzi limefia hapo,lilikuwepo zamani
Sitaki upige tena,nishafuta namba yako.

SHAIRI=NISHAFUTA NAMBA YAKO
MTUNZI=Idd Ninga wa Tengeru Arusha
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com


 
Iddi, huyo kwenye picha ni nani???

Hata sijui ulichoandika.......kama utakuwa muungwana kuniunga naye tafadhali! Nina shida nae.....
 
Ndio [HASHTAG]#Slim5[/HASHTAG]
 
Laiti ingekua mm ndo mtunzi wa shair kamwe nisingelifuta namba ya huyo kwenye pichaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…