SoC04 Nishati mbadala inavyo/itakavyo weza kupunguza/kuondoa kabisa athari za mazingira na kutufikisha katika Tanzania nzuri tuitakayo

SoC04 Nishati mbadala inavyo/itakavyo weza kupunguza/kuondoa kabisa athari za mazingira na kutufikisha katika Tanzania nzuri tuitakayo

Tanzania Tuitakayo competition threads
Joined
Apr 20, 2024
Posts
25
Reaction score
26
NISHATI MBADALA - Ni nishati safi, rafiki wa mazingira, afya ya binaadamu na wanyama. Andiko langu linalenga zaidi, MKAA/KUNI TAKA (Briquettes)/MAJIKO BUNIFU(Cooking Stoves), inayotokana na malighafi(Materials) za bure/rahisi zinazopatikana kwenye mazingira yetu bila kuathiri mazingira, malighafi hizi ambazo zinatumika katika kutengeneza nishati mbadala/safi ni kama;- oil chafu, landa za mbao, vifuu vya nazi, makaratasi, masuke ya mpunga/mahindi, vumbi la mkaa, magunzi ya mahindi, maboksi na mabaki ya mimea. Hivyo hizi taka zinaweza kutumiwa kwa kugeuzwa na teknolojia rahisi sana ili kutengeneza mkaa/kuni/nishati safi ambayo ni rafiki kwa mazingira na afya kiujumla, tofauti na mkaa au kuni zinazokatwa kutokana na malighafi za misitu, ambazo hupelekea athari hasi kwa mazingira, binaadamu/wanyama na kuathiri hali ya tabia nchi.

Kwa mujibu wa Ripoti ya Tatu ya Hali ya Mazingira nchini ya mwaka 2019, kasi ya uharibifu wa misitu ni kubwa na kila mwaka zaidi ya hekta 469,420 huharibiwa kutokana na ukataji wa miti kwa ajili ya matumizi ya kuni na mkaa. Hali kadhalika inakadiriwa kuwa asilimia 16 ya ardhi imeharibika na inakabiliwa na kuenea kwa hali ya jangwa na ukame kutokana na watu wengi kufanya shughuli zisizo endelevu ikiwemo kutumia nishati ya kuni na mkaa kwa ajili ya kupikia, kutokana na nishati hiyo kupatikana kwa urahisi na wengi wao wanaweza kumudu gharama yake. Chanzo- www.vpo.go.tz
Mhandisi Tarimo “kuna athari nyingi za kiafya kwa watumiaji wa mkaa na kuni, ambapo vifo zaidi ya watu 33,000 hutokea kwa mwaka kutokana na kuvuta hewa ya ukaa.” Chanzo- www.nishati.go.tz

Kuna wajasiliamali/vikundi (Makampuni madogo madogo), ambayo yamekuwa yakijishughulisha na kutengeneza mkaa/kuni taka (briquettes)/ Majiko bunifu. Wengine wanatambulika na wengine hawatambuliki na serikali/mamlaka husika ila wanafanya/kuzalisha mkaa taka kwa kiwango fulani kulingana na soko wanalolipata.
Kwa utafiti wangu nimeweza kuwatambua wazalishaji/watengenezaji wengi wa mkaa/kuni taka na majiko bunifu/sanifu na baazi yao ni kama;-​
  1. KuniSMART (Mwanza)- Watengenezaji/wazalishaji, kuni taka na majiko bunifu ya nishati safi.​
  2. MkaaPoa (Arusha)- Wazalishaji/watengenezaji wa mkaa taka.​
  3. Mkombozi stove (MREI- Mwanza)- Watengenezaji na wasambazaji wa majiko bunifu yanayotumia oil chafu ili kuzalisha nishati.​
  4. Mkaa wa Idris (Tabora)- Wazalishaji wa mkaa taka.​

Chanzo: Bernard Makachia (KuniSMART)


Chanzo: Bernard Makachia (KuniSMART)


Chanzo: Bernard Makachia (KuniSMART)


Ripoti ya Matumizi ya Kuni Tanzania.jpeg

Chanzo: Hali ya Upatikanaji wa Nishati 2016 (Nukta).

Mambo yafuatayo ni muhimu sana, kwa Serikali kuyatekeleza ili kuhakikisha matumizi ya nishati mbadala yanafanikiwa;-​
  1. Wazalishaji wote wa mkaa/kuni taka (Briquettes) na majiko bunifu, watambulike rasimi katika mamlaka husika ili kuwapa nguvu katika utendaji na ukuaji wao. Mamlaka kama TBS/SIDO/TIRDO/BRELLA, ziwasaidie wazalishaji katika ukuaji, kukagua, kuwaelimisha na kuwapa vibali katika bidhaa zao ili ubora ukizi soko la ndani na nje.​
  2. Serikali izipe taasisi za kifedha (Benki) nguvu kwa mkono wake kuwakopesha wazalishaji/watengenezaji wote ili kuwapa uwezo wa kukuza mitaji yao ili kuzalisha kwa kukizi hali ya soko la ndani na nje ya nchi.​
  3. Elimu itolewe kwa kila mwananchi. kuwa na kampeni juu ya nishati mbadala na jamii ifundishwe juu ya faida ya kutumia nishati safi zidi ya athari za nishati inayokinzana na mazingira.​
  4. Bei ya mkaa inayotozwa na serikali kwa kila kilo au gunia iongezwe mara mbili au zaidi ya bei elekezi ya sasa ili kuwafanya wanunuaji wa mkaa wasiweze kununua na hii itapelekea kuua soko la mkaa. kwani kwa kadri makatazo na sheria kali za kukata mkaa na kuni zinavyozidi, ndivyo uhitaji, ukuaji na uzalishaji wa mkaa taka unaongezeka.​
  5. Vibali vya uchomaji mkaa visitolewe na wale walivyo navyo wawekewe sheria ya ukomo wa hivyo vibali na baada ya muda tutakuwa hatuna vibali vya wachomaji/wauza mkaa.​
  6. Kuwa na vikundi vidogo vidogo ambavyo vitatumika kuhamasisha, kutoa elimu, kuuza kuni na mkaa safi, hasa kwa maeneo yenye uharibifu mkubwa.​
HATUA TATU ZA KUINGIZA (KUPENYESHA) MKAA/KUNI TAKA (Briquettes) & MAJIKO BUNIFU HADI VIJIJINI.
  • HATUA YA KWANZA (Phase I. 2years/ 1- 2yrs).
Serikali ihakikishe Taasisi zote za umma na binafsi, wote wanaotumia mkaa na kuni (Kampuni, Shule, Mashirika) wanaanza na kutumia nishati safi, kwa kuelemishwa na kuwekewa sheria kali zidi ya mkaa na kuni, kuingia ubia na wazalishaji kwa ajili ya kuwasambazia mkaa/kuni taka (Briquettes) na majiko bunifu. Mfumo huu ili kuweza kupenya unahitaji mfumo fuatiliaji ili kuhakikisha utekelezaji wake kukamilika ndani ya miaka miwili. Tunaanza kwanza na taasisi za kiserikali, binafsi na mifumo ya juu ili kuonyesha na kuwa mfano kwa jamii.​
  • HATUA YA PILI (Phase II. 2years/ 2- 4yrs).
Baada ya kufanikiwa hatua ya kwanza, Mfumo huu unaanza kuingizwa maeneo yote ya mjini na hapa nguvu inawekezwa katika sera na elimu juu ya athari za nishati ya kawaida na faida ya nishati mbadala,. Hivyo nguvu itawekezwa katika mikoa na wilaya yote nchini. wazalishaji wote wa nishati mbadala, waliopo katika mikoa na wilaya husika watatumika kusambaza katika maeneo husika ili kurahisisha upatikanaji na usambazaji rahisi wa nishati safi.​
  • HATUA YA TATU (Phase III. 2years/ 4- 6yrs).
Ni hatua ya mwisho baada ya kufanikiwa hatua mbili za mwanzo, msisitizo, kampeni na uelimishaji unahitajika, kwani kama tujuavyo jamii ya watu wa kijijini huamini mkaa au kuni ni bora kwa kuivisha na kupika chakula kitamu na ni nishati rahisi kwao. hivyo kwa kutumia vikundi vidogo vidogo na vyama vya kina mama zitasaidia sana kwani kama tujuavyo, vikundi/vyama vya kina mama vina nguvu katika kubadili fikra. Tunaweza kuona mfano vikoba/vibubu vile vimeshika kasi vijijini.

HITIMISHO.
Baada ya hatua tatu (Phases), kufanikiwa na kupenyesha kuni/mkaa taka na majiko bunifu, tutaweza kupata faida zifuatazo;-​
  1. Kupunguza na kuondoa athari zote za mazingira, Mabadiliko tabia nchi na afya ya binaadamu na wanyama.​
  2. Kuondoa na kudhibiti takataka, kwani uzalishaji wa nishati hii mbadala unategemea zaidi takataka ambazo hutupwa na baadae kupelekea uchafuzi wa mazingira kama oil chafu, mkaratasi, vifuu vya nazi na bati taka. Kwani takataka ni Pesa.​
  3. Kuongeza ajira, pato la mtu mmoja mmoja na wote walio katika mnyororo wa thamani, Hii inaenda sambamba na kukuza pato la taifa kwa kuweza kuuza mkaa/kuni/majiko sanifu ndani na nje ya nchi.​
  4. Kulingana na tathimini ya miaka sita kufanikiwa, tutakuwa na Tanzania bora na nzuri tuitakayo.​

KAULI MBIU.
“Tanzania Bora na Nzuri yenye Kupendeza Tuitakayo Inategemea, Nishati safi”
-Nishati Safi ni Maisha Bora na Tanzania Bora.​
 
Upvote 2
Juhudi ni nyingi sana uneonesha. Andiko ni zuri ujumbe umeufikisha.

Huu mkaa mbadala umewahi kushika umakini wangu kwa muda fulani. Nilijaribu na kweli nikatengeneza nyumbani. Nimetumia kidogo ikawa na changamoto ya uwakaji. Basi niliacha.

Lakini pia uki'search' page nyingi za watu walioanzisha miradi ya namna hiyo. Wachache niliowauliza waliachana na project. Ninaamini wana changamoto walizopitia. Utafiti unahitajika.

Lakini ikiwa kweli ni mkaa safi wenye uwakaji mzuri na gharama ndogo ya uzalishaji ni kivipi hautawali mtaani. Hivi Ford na kitengo chake cha KINGSFORD Briquetes waliwezaje?

Nitoe rai kwa utafiti unaosimamiwa kitaifa kuona changamoto zinapatiwa ufumbuzi. Narudi kwenye jeshi letu. Military science department hasa za Iringa na kwingine penye mbao zinaweza kufanya project ya kuboresha huo mkaa usiishie kuwa wa maonyesho tu. Kama jeshi likawa na mkaa spesho wa kiwango wa briquette.

Ni kwa nini nimekazia kwa jeshi. Kwa kweli ninaona hayo ndiyo matumizi bora zaidi ya unga wa risasi na mabomu katika kipindi hiki cha amani. Tanzania ni kisiwa cha amani. Teknolojia na zitusaidie sasa hivi. Mzinga mpo wapi? Kama tu mnavyozalisha baruti kwa ajili ya nchi ivune madini. Vivyo hivyo tunaweza kuboresha mkaa huu nchi ikapata hewa safi. Ahsanteni.
 
Back
Top Bottom