Tangawizi
JF-Expert Member
- Jun 25, 2009
- 6,696
- 6,734
Baada ya kutembelea sehemu mbalimbali za nchi yetu, ni wazi tulipo sasa tumeshaka karibu miti yote kwa ajiri ya kutengenezea mkaa ambao unatumika kama nishati kwenye nyumba nyingi kuanzia vijiji mpaka mijini. Kwa bahati mbaya hatukukata miti kwa mipango endelevu ya kupanda mingine ili tusijefika sehemu tukawa hatuna miti kabisa ya kukata.
Nimekaa na kujiuliza sana hivi nini itakuwa nishati mbadala kwa ajiri ya matumizi ya nyumbani, vijijini na hata mijini.
Ilivyo leo, gas imeanza taratibu kushika kasi ingawa bado kuna vikwazo vingi katika kuhakikisha watu wengi zaidi wanaitumia kama chanzo cha nishati. Mfano, leo hii matumizi ya gas yamekuwa makubwa na storage ya LPG nchini ni kama zimebaki vilevile. Hii inapelekea gas kukosekana na kuishiwa kulangua mpaka kufikia bei ya juu sana. Wengi hatutaweza kuzimudu hizi bei kama zitaendelea hivi zilivyo.
Makaa ya mawe yapo ingawa hatujui nini cha kufanya nayo, au bado tunapanga deal ya namna ya kuneemeka nayo kwa wale walio karibu na kitoweo hicho!
Umeme sote tunajua jinsi unavyotumika kama sehemu ya kujitajirisha kwa haraka haraka kwa watu wenye mamlaka ingawa wananchi tunapata shida kubwa za mgao usiokoma.
sasa jamani nishati ipi itakuwa ndio mbadala kwa matumizi ya nyumbani maana kwa speed hii ya kukata miti nina shaka kama tutafika mbali sana bila kujikuta tuna shida kubwa ya upatikanaji wa mkaa