SoC02 Nishati mbadala zitokanazo na takataka za karatasi

Stories of Change - 2022 Competition

mtozatozo

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2021
Posts
459
Reaction score
415
UTANGULIZI:

Kumekua na mabadiliko makubwa ya Tania nchi ktk sayari yetu kwa miaka ya hivi karibuni .Miongoni mwa sababu kubwa ya mabadiliko hayo yaletayo athari mbalimbali Kama mafuriko,ukame na kadhalika,ni uchafuzi wa mazingira utokanao na shughuli mbalimbali Kama ongezeko kubwa la viwanda,magari mengi yanayitumia nishati ya dizeli na petroli, shughuli za kilimo pembezon mwa kingo za mito zinazosababisha mmomonyoko wa undongo na hatimaye kufanya mkondo wa mto kujaa udongo na maji kusambaa ovyo bila muelekeo wake wa asili,utupaji takataka ovyo(madampp yasiyo rasmi)hivyo kuleta sio tu mabadiliko ya tabia nchi,Bali hata Mandhari mbaya katika miji yetu na mazingira yote kwa ujumla tunayoishi.

Mifano michache ni eneo la jangwani kugeuzwa dampo lisilo rasmi na wafanyabiashara wa madafu na miwa kwenda kutupa mabaki na uchafu baada ya kumaliza biashara zao.Pia kando ya bonde lote la mto Msimbazi kumegeuzwa dampo na wakazi waishio pembezon mwa mto huo.

Kumekua na jitihada mbinu mbalimbali za kunusuru sayari yetu dhidi ya mabadiliko hayo ya tabia nchi,hasa sababu zile zitokanazo na shughuli za kibinadamu katika uchafuzi wa mazingira.Miongoni mwa jitihada hizo ni pamoja na kupiga marufufuku matumizi ya mifuko ya plastiki maarufu kama rambo,ambayo katika miaka michache iliopita ilileta tishio kubwa katika mazingira duniani kwa ujumla(nchi kavu na baharini)pia kumekua na mpango wa kurejea matumizi kwa bidhaa za plastiki kwa kukusanya takataka za plastiki mitaani,kuziyeyusha na kutengeneza bidhaa mpya za plastiki.Mbinu hizi na jitihada hizo kiukwel zimeleta matumaini makubwa kwa siku za mbeleni kuokoa mazingira yetu, pamoja na kuja teknolojia ya magari yatumiayo gesi asilia,na magari yatumiayo umeme.

MADA:
Hivyo basi,pamoja na jitihada zote hapo juu kwa serikali,mashirika yasiyo ya kiserikali,taasisi mbalimbali,makampuni, mashirika ya kimataifa pamoja na watu binafsi,nami nimekuja na wazo litakalosogeza jitihada hizo hatua moja kwenda nyingine.Miongoni mwa mamilioni ya tani za takataka zinazozalishwa kila siku duniani,zipo takataka zinazotokana na bidhaa za karatasi Kama vile vifungashio vya bidhaa mbalimbali pamoja na maboksi,ambayo kwa wingi yamekua yakizagaa ovyo mitaani na kuleta picha mbaya kwa majiji na miji yetu.Ipo namba ya kukusanya takataka hizi na kuzifanya zitumike Tena nakuleta faida kubwa katika jamii yetu.Mnyororo mzima wa uongezaji thamani katika biashara hiyobutaleta usafi wa mazingira,ajira na kusisimua uchumi

MAZINGIRA;
Kwakua upatikanaji wa malighafi wa bidhaa zetu utatokakana na makaratasi na maboksi, ambayo kwa kiwango kikubwa yamezagaa sehem mbalimbali mitaani, hivyo basi ukusanyaji wa malighafi yetu moja kwa moja utaleta athari chanya kwenye mazingira yetu kwa kuyaacha Safi.Mfano mdogo ni eneo la kariakoo ambako kila siku magari ya kubeba takataka lazima yapite kukusanya maboksi na vifungashio mbalimbali ambavyo hupelekwa dampo.kwahyo uhitaji wa magari ya kubeba takataka katika maeneo hayo yatapungua kwa kiasi fulani na kuelekezwa sehem nyingine.

AJIRA:
Serikali bado imekua ikipambana kutokomeza 'janga' la ukosefu wa ajira miongon mwa raia wake(hasa vijana)hivyo basi kumekua na jitihada mbalimbali za kujikwamua na janga Hilo kwa vijana na akina mama kubuni namna mbalimbali za kujiajiribna kujikwamua kiuchumi kwao na wategemezi wao.Mionngoni mwa jitihada hizo ni pamoja na kuokota makopo,ambapo kama tulivyoona hapo awali hutumika kutengeneza upya bidhaa za plastiki.Pamoja na kupata kipato Chao binafsi,lakini pia hutusaidia katika usafi wa mazingira.Mpango huu nilionao utaongeza wigo wa usafi wa mazingira na kipato pia kwa wale watakaojishughulisha na uokotaji huk.Kwa mfano,kwa hali ilivyo sasa,muokotaji huyo ataokota chupa za plastiki tu,hawezi kuokota karatasi au boksi kwakua Hana sehem ya kuzipeleka, lakin Kama wazo langu litafanikiwa kupenya na kufanya kazi katika jamii,itaongeza chachu ya ukusanyaji wa aina hiyo ya takataka kwani muokotaji tayari atakua na uhakika wa kwenda kuziuza sehem fulani.

BIASHARA YENYEWE:
Kwa utafiti nilioufanya,upo uwezekano wa kubadilisha takataka zitokanazo na bidhaa za karatasi na kua NISHATI YA KUPIKIA.Makaratasi na maboksi yaliyookotwa kutoka miataani yatalowekwa kwa muda wa siku tano, baada ya kulowekwa kwenye maji kwa muda huo,yatapondwa (mfano wa kutwanga kisamvu kwenye kinu)na kulainika vizuri,baada ya zoezi hilo,mchanganyiko huo utakamuliwa ili kuondoa kiasi kidogo Cha maji yaliyosalia kutoka kwenye kulowekwa(hapa itachukuliwa kwa mkono na kufinyangwa kwa nguvu,mfano wa tonge la ugali)baada ya zoezi hilo ambapo Sasa tutakua tumepata mabonge mfano wa tonge la ugali,hapo tutayaanika juani mfululizo kwa siku mbili hadi tatu kulingana na ukali wa jua.Baada ya kukauka vizuri hapo bidhaa yetu itakua tayari kwa matumizi.

Ubora wa nishati hii ukitofautisha na kuni au mkaa, yenyewe haitoi moshi kabisa,pia hudumu ikiwa na moto kwa muda mrefu kabla ya kua majibu.Kama tulivyoona tangu mwanzo,mchakato mzima wa utengenezaji wa bidhaa hii,una faida tele kimazingira na kiuchumi.Pia kuunga mkono juhudi za serikali na mashirika mbalimbali ya kimataifa katika jitihada za utunzaji wa mazingira,kujikimu kimaisha pamoja na kupunguza umasikini miongoni mwa wanajamii.

Kwa kuzingatia yote hayo ndugu zangu ninaomba mnipigie kura kwa wingi ili kuwezesha andiko langu liweze kushinda katika mashindano ya mwaka huu.Natanguliza shukrani zangu za dhati kwako wewe uliotumia muda wako kusoma andiko hili.ASANTENI SANA!
 
Upvote 2

Chifu Sanze ESPRESSO COFFEE Mzee Wa Kazi Chafu bagamoyo Mu congomani Taavid green rajab
 
Back
Top Bottom