Nishati: Petroli yashuka kwa Tsh. 116, Dizeli Tsh. 148 Dar, Mafuta ya Taa yabaki palepale

Very simple.. mfano Tu petrol kwa dar gharama wamesema zimeshuka 30% je shillingi 116 no % 30 ya 3274 tulokuwa tukinunua kwa Lita?? Jibu no kuwa bado watu wanakula parefu...

Pia nauli kupanda hii in December watu wanataka maokoto ya chap chap.. wanaitaga mwez wa Neena kwao huu.. so wameshahonga
 

Mwigulu na pHd yake ambayo leo si mjadala, ndiye aliyeshauri serikali na baraza la mawaziri wasijichoshe kukusanya fedha, waweke kodi kwenye mafuta na miamala, maana matajiri hawana tabia ya kulalamika na si wapiga kura huku maskini wakibaki kushangilia kodi kulipwa na matajiri.

Bei kikomo za mafuta November 2023 petroli imeshuka kwa Sh.7 na dizeli imeshuka kwa Sh.74September 2023 bei ya mafuta ya petroli ilipanda kwa zaidi ya Sh500 (17%) kwa lita moja.

Serikali ya Tanzania ina matusi kwa wananchi. Hawajali hali za wananchi. Mnapongeza tu.Mwezi mmoja kabla Samia kuingia madarakani Feb 2021 lita 1 ya petroli iliuzwa Sh1,887.

July 2023 lita 1 ya petroli ikauzwa Sh2,736 Samia Suluhu Hassan akiwa na miaka 2 madarakani.
Wanaosema mafuta yameshuka bei, watueleze lita 1 tunaipata chini ya Sh1,887 aliyoikuta Samia?

Tukikosoa, tunataka unafuu wa maisha. Mnaopengeza, mnanufaika na huu ugumu wa maisha?Katika soko la Dunia, Oktoba, pipa 159lt limeuzwa Sh219,175. 1lt Sh1,399.

Uagizaji ni Sh89/ltBandari ya DSM 1lt inafika kwa Sh1,488. Kwanini DSM wauziwe 1lt kwa Sh3,158? (ongezeko Sh1,670).Mteja analipa Sh1,670 gharama ya tozo za serikali. Tozo ni zaidi ya nusu ya bei ya bidhaa katika pampu.

Kuliko kumwaga pongezi kwa kupunguza shilingi MIA katika lita ya mafuta, waambie waondoe TOZO.Hakuna kinachoshindikana petroli kuuzwa Sh.2,000 kwa lita moja katika pampu (vituo vya mafuta).Tozo na kodi katika bidhaa za mafuta ya petroli, dizeli na kerosene zipo 23 jumla yake Sh. 2,405.

Tukiondoa tozo β€˜mshenzi’ petroli - bei soko la Dunia ni Sh1,375 kwa lita, mafuta yatashuka zaidi. Mafuta ya petroli (Sh3,158) na dizeli (Sh3,226) kwa kwa lita bado ni ghali sana. Punguza pongezi​
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…