Nishati Safi: Je ni busara ya kuendelea kutumia ruzuku ili kusambaza mitungi ya gesi wakati ni gharama na kuna mbadala

Nishati Safi: Je ni busara ya kuendelea kutumia ruzuku ili kusambaza mitungi ya gesi wakati ni gharama na kuna mbadala

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Nimeona hii qoute ya habari

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Nishati Jadidifu na Teknolojia Mbadala akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa REA, Mha. Advera mwijage amesema mitungi ya gesi 452,445 yanye gharama ya shilingi bilioni 8.64 inakwenda kusambazwa nchini ambapo kila wilaya itapata mitungi 3,255.

Swali linakuja Kwanini tunafanya hivyo wakati tuna mbadala ambao ni gharama nafuu na tunazalisha wenyewe wakati hii gesi sio yetu tunaagiza ?





Hitimisho
Je ni kwamba Hatufahamu haya au kuna faida gani tunapata ? Au ni kipi sijaelewa... Yaani tunahamasisha kitu ambacho....
  1. Kina gharama kuliko mbadala
  2. Sio cha kwetu tunaagiza kutoka nje
  3. Mbadala tunao
  4. Tunakata pesa kwenye mbadala (Kodi) ili mbadala upande gharama (Umeme) ili tuweke Ruzuku pengine.., mbaya zaidi huko pengine wala sio mali yetu (watu binafsi na mataifa ya nje)
  5. Tunakataza watu kutumia wanachotumia sasa (kuni) ambazo ni bure kwa kuwapa mitungi ambayo ina gharama zaidi ya 200/= kuliko tungewaambia watumie Umeme (Hatuwaambii ukweli) na hata tukiwapa Ruzuku ni kwamba Kodi zao ambazo zingetumika pengine ndio tunazipeleka huku kwenye Gesi.
 
Watu wanatumia hiyo gesi ikiisha wanauza mitungi au wanaweka ndani forever.
 
Watu wanatumia hiyo gesi ikiisha wanauza mitungi au wanaweka ndani forever.
Bado ni matumizi ya Kodi zao.., bora wangewapa hizo pesa sababu wakiuza hawawezi wakauza kama bei ya soko...

Cha kuwauliza hao wakija kugawa ni rahisi sana..,
  • Je hayo ndio matumizi bora ya Kodi zetu ?
  • Kwanini kama ni ruzuku msitupe majiko ya umeme sababu mwisho wa siku huenda isiwe bure kama kuni bali bado ni nafuu kuliko kujaza gesi
  • Kwanini tusitumie cha kwetu (LPG tunaagiza)
  • Hio Ruzuku mnayotoa huku je mnaipunguza wapi ?
  • Mwisho wa kugawa hizi Ruzuku ni lini au mkiacha kugawa kugawa hio mitungi watu turudi kwenye kuni ?
 
Back
Top Bottom