Tukuza hospitality
JF-Expert Member
- Jul 30, 2022
- 321
- 691
Utangulizi
Ni ukweli kuwa swala la nishati safi ya kupikia limekuwa linapigiwa chapuo kwa miaka mingi na serikali pamoja na wadau wengine mbalimbali, yaani watu binafsi na asasi za kiraia. Tangu utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius K. Nyerere hadi sasa, swala la nishati safi limekuwa agenda muhimu, ambapo miradi mbalimbali imekuwa ikitekelezwa. Ni ukweli usiopingika kwamba, pamoja na jitihada zote hizi, mpaka leo ni wananchi (wa vijijini na mijini) chini ya asilimia kumi wanatumia nishati safi!
Katika maeneo mengi nchini, hasa vijijini, kuna maradhi mbalimbali kama malaria, kuhara na mengine, ambapo wahanga wakubwa ni watoto. Maeneo ambayo uelewa ni mdogo juu ya maradhi haya huyahusianisha na imani za kishirikina. Kutokana na hali hii, wagonjwa hawapelekwi katika vituo rasmi vya afya, jambo linalosababisha vifo, hasa kwa watoto.
Matumizi ya nishati ya kuni kwa muda mrefu husababisha maradhi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ya macho. Wahanga wakubwa ni wanawake, ambapo macho yao huwa mekundu. Wanawake hawa, hasa kutoka kanda ya ziwa, wanaadhibiwa mara tatu: kwanza, kutafuta kuni kwa tabu kila siku kwa miaka mingi; pili, kuumizwa na moshi wa kuni kwa miaka mingi na hivyo kuwa na macho mekundu; na tatu, kuuawa na watu wao wa karibu kwa tuhuma za kuua watoto wao kichawi, kumbe watoto wanakufa kwa magonjwa ya kawaida ambayo yangetibika katika vituo vya afya.
Serikali, kwa kushirikiana na wadau wengine, iwezeshe taasisi zake zote, kama shule za msingi (ambazo zimesambaa karibu kila kijiji hapa nchini), shule za upili, na vyuo kutumia nishati safi, hasa gesi asilia na/au bayogesi. Hii italeta taathira chanya na kubwa nchini kwa muda mfupi, kwani wananchi wanaozunguka taasisi hizi watajifunza na kufahamu umuhimu wa nishati safi na hivyo kuanza kuitumia katika kaya zao.
Sambamba na hili, serikali ipunguze kodi na hata kuweka ruzuku katika vifaa/zana za nishati safi, pamoja na nishati yenyewe, hasa umeme na gesi asilia. Pia, serikali kwa kushirikiana na wadau wengine, watengeneze mfumo (sera na sheria) ambao utalazimisha kila taasisi kuingiza swala la nishati safi katika mipango yake ya maendeleo, na kutolea taarifa kila mwezi, robo mwaka, nusu mwaka, na mwaka.
Mbali na kutunza mazingira, kunusuru afya za watu hasa wanawake vijijini, mkakati huu utachochea uzalishaji katika viwanda vidogo, vya kati na vikubwa, na hivyo kuuchochea uchumi wa mtu mmoja mmoja na wa taifa kwa ujumla.
Hitimisho
Nishati safi kwa kila Mtanzania inawezekana endapo serikali itaibeba kama agenda ya kimkakati na mtambuka kwa ngazi zote za serikali, pamoja na sekta binafsi.
Ni ukweli kuwa swala la nishati safi ya kupikia limekuwa linapigiwa chapuo kwa miaka mingi na serikali pamoja na wadau wengine mbalimbali, yaani watu binafsi na asasi za kiraia. Tangu utawala wa awamu ya kwanza ya Mwalimu Julius K. Nyerere hadi sasa, swala la nishati safi limekuwa agenda muhimu, ambapo miradi mbalimbali imekuwa ikitekelezwa. Ni ukweli usiopingika kwamba, pamoja na jitihada zote hizi, mpaka leo ni wananchi (wa vijijini na mijini) chini ya asilimia kumi wanatumia nishati safi!
Madhara ya Kutotumia Nishati Safi
Kiafya
Kutotumia nishati safi husababisha maradhi mbalimbali katika mfumo wa upumuaji. Maradhi haya ni mengi katika maeneo ya vijijini ambapo kwa kiasi kikubwa watu wanatumia nishati ya kuni. Matumizi makubwa ya nishati hii pia husababisha maradhi ya macho.Mazingira
Ukataji miti kwa ajili ya kuni na mkaa kwa kiasi kikubwa umeharibu mazingira na hivyo kusababisha mabadiliko ya tabia nchi nchini Tanzania na nchi nyingine nyingi duniani. Tumeshuhudia vimbunga, mafuriko na ukame. Majanga haya yamesababisha njaa, maradhi mbalimbali, na hata vifo.Kijamii
Baadhi ya maeneo hapa Tanzania, hasa vijijini, kuna uhaba wa nishati ya kuni. Hii husababisha wanawake wengi kutumia muda mrefu kupata nishati hii, na hivyo kupunguza muda wa uzalishaji na wa kuhudumia familia. Pia, kwa kuwa wanawake ndio wanahusika kupika chakula cha familia kwa mujibu wa mila na desturi zetu, wengi wao ndio waathirika wakubwa wa magonjwa yanayotokana na matumizi ya nishati ya kuni/mkaa, ikiwa ni pamoja na magonjwa ya macho. Katika maeneo ya kanda ya ziwa, hasa mikoa ya Shinyanga na Simiyu, kwa muda mrefu limekuwa na matukio ya mauaji ya wanawake wazee kwa tuhuma zinazotokana na imani za kishirikina. Watekelezaji wa mauaji haya ni ndugu wa karibu wa wanawake hawa (ikiwa ni pamoja na watoto au wajukuu wao). Kielelezo kinachotumiwa na wauaji hawa ni macho mekundu.Katika maeneo mengi nchini, hasa vijijini, kuna maradhi mbalimbali kama malaria, kuhara na mengine, ambapo wahanga wakubwa ni watoto. Maeneo ambayo uelewa ni mdogo juu ya maradhi haya huyahusianisha na imani za kishirikina. Kutokana na hali hii, wagonjwa hawapelekwi katika vituo rasmi vya afya, jambo linalosababisha vifo, hasa kwa watoto.
Matumizi ya nishati ya kuni kwa muda mrefu husababisha maradhi mbalimbali, ikiwa ni pamoja na ya macho. Wahanga wakubwa ni wanawake, ambapo macho yao huwa mekundu. Wanawake hawa, hasa kutoka kanda ya ziwa, wanaadhibiwa mara tatu: kwanza, kutafuta kuni kwa tabu kila siku kwa miaka mingi; pili, kuumizwa na moshi wa kuni kwa miaka mingi na hivyo kuwa na macho mekundu; na tatu, kuuawa na watu wao wa karibu kwa tuhuma za kuua watoto wao kichawi, kumbe watoto wanakufa kwa magonjwa ya kawaida ambayo yangetibika katika vituo vya afya.
Kisiasa
Mauaji ya wanawake wazee kutokana na imani za kishirikina yanayotokea zaidi katika maeneo ya kanda ya ziwa yamekuwa yakizua taharuki kwa wananchi, pamoja na viongozi wa serikali. Miaka ya sabini, aliyekuwa waziri wa mambo ya ndani, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, alilazimika kujiuzulu kufuatia mauaji ya wananchi (hasa wanawake) mkoani Shinyanga kutokana na imani za kishirikina. Naamini wapo watu wengine waliokuwa chini yake waliwajibika au kuwajibishwa kutokana na matukio hayo. Waziri huyu (A. H. Mwinyi), ndiye alikuja kuwa Raisi wa awamu ya tatu Zanzibar, na Raisi wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Tanzania Tuitakayo 2025 - 2050, Katika Swala la Nishati
Nimefuatilia bajeti ya 2024/2025 iliyowasilishwa bungeni tarehe 13/06/2024; sikuona mpango mkakati wa kuinua matumizi ya nishati safi kwa mwananchi wa Tanzania. Badala yake, serikali inapanga kuongeza kodi katika vyombo vya usafiri vinavyotumia nishati ya gesi asilia na ya umeme!Swala la Nishati Safi, Liwe Mtambuka na la Kimkakati
Kila sekta ya serikali inapaswa kuingiza swala la nishati safi katika mipango yake ya maendeleo, kuanzia ngazi ya serikali kuu, mpaka ngazi ya serikali za mitaa. Nishati safi zilizopo nchini ambazo hazitumiki kikamilifu ni umeme, gesi asilia, na bayogesi (gesi inayotokana na vinyesi vya binadamu na wanyama).Serikali, kwa kushirikiana na wadau wengine, iwezeshe taasisi zake zote, kama shule za msingi (ambazo zimesambaa karibu kila kijiji hapa nchini), shule za upili, na vyuo kutumia nishati safi, hasa gesi asilia na/au bayogesi. Hii italeta taathira chanya na kubwa nchini kwa muda mfupi, kwani wananchi wanaozunguka taasisi hizi watajifunza na kufahamu umuhimu wa nishati safi na hivyo kuanza kuitumia katika kaya zao.

Upvote
9