Nishati Safi ya Kupikia: Kwa Kutumia Tariff Zero (100 per Unit) Mpikiaji badala ya kutumia Gesi Ataokoa Tshs 206/= kwa kila unit

Nishati Safi ya Kupikia: Kwa Kutumia Tariff Zero (100 per Unit) Mpikiaji badala ya kutumia Gesi Ataokoa Tshs 206/= kwa kila unit

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Yaani kila mwanakijiji au kama tukiamua wote wawe Tariff Zero kila mwenye Mtungi wa kujaza elfu 25 akienda kununua huyu wa umeme anasave elfu 16 au kwa maana nyingine ni kama mwenye umeme ananunua mtungi wa gesi kwa elfu nane. Hili lipo wazi kabisa swali ni kwamba kwanini kama Taifa tunapigia chapuo gesi?

Umeme ni kama Maji kwenye Bomba ukifungulia lazima utumike au Unaupoteza; Kuliko kuuzia watu Umeme kwa Tariff ya Kawaida 292/= na Wengi kuwaunganisha na Tariff Zero Tshs 100/= na Wakaongeza Matumizi kwa Kupikia Utakuwa bado una Makusanyo yaleyale, Matumizi yaleyale na Kupunguza Gharama kama Taifa la Kutumia fedha za Kigeni kuagiza Gesi ya Kupikia.

Nishati ikizalishwa lazima itumike au inapotea mfano nishati ya maji kama ile nguvu ya maporoko ya maji yanaweza kuzalisha 2kw kwa kila saa na wewe ukiwa unatumia 1kw ni kwamba nusu ya Nishati inapotea na sio kwamba unakuwa umeokoa gharama...., hivyo kwa kupunguza Bei badala ya kuongeza, utakuwa umeongeza watumiaji wa Umeme kupikia hivyo kuokoa gharama ya uagizaji wa gesi na kumpunguzia matumizi mtumiaji pesa ambayo atatumia kwa mambo mengine.

Badala ya kuingia kwenye Mitego ya Kuingia Mikataba na Madalali (so called wawekezaji) hivyo gharama ya Umeme Kupanda kwanini tusisimamie kama Taifa na Kipaumbele kiwe gharama nafuu kwa mtumiaji ?
Umeme ni Huduma na mafanikio yanapimwa kwa gharama affordable kwa mtumiaji na sio Makusanyo ya Serikali ambayo in the first place dhima yake ni kutoa Huduma, hivyo kama ni uwekezaji basi uwe kwenye uzalishaji na yoyote anayeweza kuzalisha na azalishe so long as atauzia Tanesco bei rahisi kuliko Tanesco anayoweza kuzalisha na kwa karne ya sasa kuna uwezekano wa kila raia akawa mzalishaji.

Njia Pekee ya kuingia kwenye Nishati Safi ya Kupikia kwa Gharama Ndogo ni Umeme Tuwekeze Nguvu zetu zote huko, Kuagiza Gesi ni Ulimbukeni na Kama Gesi ni rahisi basi isipelekwe Majumbani bali kwenye Kufua Umeme ili izalishe Umeme (After all tuna Gesi ya Mtwara)

Kinachoendelea ni kukosa Uzalendo kwa watu kwa ajili ya biashara zao kupigia chepuo kitu ambacho kina gharama (gesi) kuliko alternative (umeme) rai yangu kwa watu hawa angalau mara moja waangalie ustawi wa nchi na sio ustawi wao.., na kama ni biashara na kufukuzia fursa basi wawekeze kwenye kuuza vifaa vya umeme au hata kuzalisha umeme kama wanaweza kuwa na bei nafuu kuliko Tanesco.

Kwahio next time mbunge wako au Waziri akikuletea Mtungi wa Gesi bure mwambia Asante sana ila tashukuru zaidi kama unikipigania gharama ya Umeme ikashuka kwa kufanya hivyo utaokoa pesa zangu za kodi unazotumia kuagizia hii gesi unayonipa ili kila nikinunua nipoteze Tshs 16,000/= na zaidi.

Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichonacho na Tufanye Tunachoweza...
 
Yaani kila mwanakijiji au kama tukiamua wote wawe Tariff Zero kila mwenye Mtungi wa kujaza elfu 25 akienda kununua huyu wa umeme anasave elfu 16 au kwa maana nyingine ni kama mwenye umeme ananunua mtungi wa gesi kwa elfu nane.... Hili lipo wazi kabisa swali ni kwamba kwanini kama Taifa tunapigia chapuo gesi ?

Umeme ni kama Maji kwenye Bomba ukifungulia lazima utumike au Unaupoteza; Kuliko kuuzia watu Umeme kwa Tariff ya Kawaida 292/= na Wengi kuwaunganisha na Tariff Zero Tshs 100/= na Wakaongeza Matumizi kwa Kupikia Utakuwa bado una Makusanyo yaleyale, Matumizi yaleyale na Kupunguza Gharama kama Taifa la Kutumia fedha za Kigeni kuagiza Gesi ya Kupikia
Nishati ikizalishwa lazima itumike au inapotea mfano nishati ya maji kama ile nguvu ya maporoko ya maji yanaweza kuzalisha 2kw kwa kila saa na wewe ukiwa unatumia 1kw ni kwamba nusu ya Nishati inapotea na sio kwamba unakuwa umeokoa gharama...., hivyo kwa kupunguza Bei badala ya kuongeza, utakuwa umeongeza watumiaji wa Umeme kupikia hivyo kuokoa gharama ya uagizaji wa gesi na kumpunguzia matumizi mtumiaji pesa ambayo atatumia kwa mambo mengine

Badala ya kuingia kwenye Mitego ya Kuingia Mikataba na Madalali (so called wawekezaji) hivyo gharama ya Umeme Kupanda kwanini tusisimamie kama Taifa na Kipaumbele kiwe gharama nafuu kwa mtumiaji ?
Umeme ni Huduma na mafanikio yanapimwa kwa gharama affordable kwa mtumiaji na sio Makusanyo ya Serikali ambayo in the first place dhima yake ni kutoa Huduma, hivyo kama ni uwekezaji basi uwe kwenye uzalishaji na yoyote anayeweza kuzalisha na azalishe so long as atauzia Tanesco bei rahisi kuliko Tanesco anayoweza kuzalisha na kwa karne ya sasa kuna uwezekano wa kila raia akawa mzalishaji

Njia Pekee ya kuingia kwenye Nishati Safi ya Kupikia kwa Gharama Ndogo ni Umeme Tuwekeze Nguvu zetu zote huko, Kuagiza Gesi ni Ulimbukeni na Kama Gesi ni rahisi basi isipelekwe Majumbani bali kwenye Kufua Umeme ili izalishe Umeme (After all tuna Gesi ya Mtwara)
Kinachoendelea ni kukosa Uzalendo kwa watu kwa ajili ya biashara zao kupigia chepuo kitu ambacho kina gharama (gesi) kuliko alternative (umeme) rai yangu kwa watu hawa angalau mara moja waangalie ustawi wa nchi na sio ustawi wao.., na kama ni biashara na kufukuzia fursa basi wawekeze kwenye kuuza vifaa vya umeme au hata kuzalisha umeme kama wanaweza kuwa na bei nafuu kuliko Tanesco

Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichonacho na Tufanye Tunachoweza...
Hii tarrif zero tuliochelewa kuistukia wanatubania kuunganisha
 
Hii tarrif zero tuliochelewa kuistukia wanatubania kuunganisha
Kwanza kwa walio nayo inafutwa na kubakia vijijini pekee na walivyo mashetani badala ya kuwaambia vijijini kwamba ni gharama kutumia gesi wanawapa mitungi na kuwakataza kutumia Kuni..., Yaani ni kama Drug Dealers wanatafuta Mateja....

Kwahio unless upo kijijini basi ni haki yako unless otherwise cha kufanya ni kuwashinikiza hawa wabunge wetu waliogeuka kuwa watetezi wa serikali washinikiza bei zishuke
 
Ukiona wanasiasa wanapigia sana kelel jambo fulani, ujue wana maslahi nalo, kama jambo lina maslahi na wananchi bila maslahi yao, huwezi kuona wanaleta visura sura vyao vya wizi.
 
Ukiona wanasiasa wanapigia sana kelel jambo fulani, ujue wana maslahi nalo, kama jambo lina maslahi na wananchi bila maslahi yao, huwezi kuona wanaleta visura sura vyao vya wizi.
Dawa ni kuhakikisha angalau wenye nchi (wananchi) wanakuwa knowledgeable hivyo wakileta hizi blah blah blah waweze kuwauliza maswali ya kina..., Ila haya ni mauaji ya hali ya juu kucheza na Nishati ni kuingilia maisha ya kila mbangaizaji..., mbaya zaidi unapomdanganya mtu kwa kumpa kitu cha bei mbaya kuliko anachotumia au angeweza kutumia tena kwa kutumia Kodi zake ni Mauaji ya hali ya juu... for what ? Vijisenti vya hapa na pale ?

Hopefully nawapa benefit of doubt kwamba ni naivete na sio malevolence
 
Hapa kuna watu watakuja kutetea chama badala ya maslahi ya nchi. Wanasahahu chama kinaweza kufa muda wowote lakini Taifa likabiki milele labda waamuele kuuza kama Mangungo wa Msovero.
 
1kg ya Gesi = 13.6kwh (units)
Kwenye Mtungi wa 6 kgs (
ingawa gesi iliyopo kwenye mtungi sio 6kgs kutokana na uzito wa Mtungi)
Kwahio kwenye Mtungi wa gesi wa 6kgs kuna Units Ngapi

13.6kwh x 6 equals to approx = 81.6 Units
Kwahio Mtungi wa kilo 6 una Units takriban 81.6

Mtungi huu unajazwa kwa Tshs. 25,000/=; Hivyo tunaweza kusema Unit moja unanunua kwa 25,000/81.6 = 306.3
Kumbuka kwa sasa
  • Unit moja mjini unanunua kwa Tshs. 292 /=
  • Vijijini Unit Moja inanunuliwa kwa Tshs. 100/=
 
Duh siwapunguze wafanye hata 200 kwa unit diferent kati ya Mjini na kijiji ni kubwa mno hata mjini kuna masikini!
 
Duh siwapunguze wafanye hata 200 kwa unit diferent kati ya Mjini na kijiji ni kubwa mno hata mjini kuna masikini!
Pote wafanye hata chini ya Tshs 100/ umeme ukishazalisha lazima utumike na kama wakimaliza Bwawa Capacity itakuwa zaidi ya mara mbili...

Ni kama mtu una mapipa kumi yanayovuja unaenda kununua kwa jirani maji (gesi) ili uwauzie majirani zako sababu maji yako unauza bei mbaya..., kwanini usipunguze bei ili maji yako yatumike badala ya kuvuja na uache kumtajirisha jirani yako..., ukizingatia hizo pesa za kununua maji ya jirani (gesi) yanamfaidisha dalali (mbeba maji) na wala sio wanakijiji pia yanafirisi nyumba yako
 
Screenshot_20250122_224343_WPS Office.jpg

Whatsapp: 0612607426
 
Back
Top Bottom