Nishati Safi ya Kupikia (Ushauri kwa Watunga Sera)

Nishati Safi ya Kupikia (Ushauri kwa Watunga Sera)

Logikos

JF-Expert Member
Joined
Feb 26, 2014
Posts
15,460
Reaction score
24,233
Kama Mwananchi nimeamua kufanya my Civic Duty..., Tumepata bahati sana wakati huu Dunia nzima imejikita kwenye Nishati Safi, hivyo kuna Pesa za Kumwaga ambazo either tutazitumia vizuri na kuwanufaisha wananchi na vizazi vijavyo kwa kujenga / kuanzisha kitu ambacho kitatusaidia milele na milele au tutazifuja na kuzitapakaza ambapo kesho yetu itakuwa haina tofauti na leo.

cover page.jpg

Kwahio nimeandaa hili jarida PDF.. (attached hapo chini) Nishati Safi ya Kupikia kwa Gharama ya Kuanzia Tshs 0/= likielezea njia ambayo tunaweza kuchukua na ikatufikisha huko au tukichukua njia nyingine huenda tukarudi nyuma au tusitatue tatizo kwa gharama ya pesa nyingi sana...; Kwenye Jarida hilo kuna uwezekano wa Mwanakijiji akaweza kuanza kupikia bila gharama ya kifedha jambo ambalo kwake itakuwa rahisi kuliko kumwambia aache kutumia kuni (bure) na atumie gesi (pesa) ambazo hana.

Kwahio nimeweka hili hapa ili wawikilishi wetu (wabunge) au mtu yoyote anaweza akacheki na kuangalia kama kinachoongelewa humu ni pumba au mchele na kama ni pumba ni vipi tunaweza kupata mchele, hivyo kama wewe una namba ya mbunge wako unaweza ukamtumia aweze kuona, sababu kama tukienda huku naposema.., faida itakuwa ya kila Mtanzania na vizazi vijavyo, na kama tukiamua kwenda huko tunapokwenda sasa hivi, Binafsi naona kama tunapotea na tunapoteza bahati ya kutumia hizi pesa zilizopo sasa kufanya jambo ambalo litakomboa Taifa letu.

Tuanzie Tulipo, Tutumie Tulichonacho na Tufanye Tunachoweza.
 

Attachments

Hivi humu tuna wabunge ?
Bwana Pasco Mayalla kuna kipindi uligombea siku ukirudi au ukiingia Kundini usisite kuwasaidia wananchi wako kwa Nishati ambayo haitawahitaji kila wakati kutoboka mifuko....
 
Dkt. Gwajima D
Nishati ikiwa ni moja ya jambo muhimu sana katika Ustawi wa Jamii nadhani tutakubaliana kuhakikisha tunapata suluhisho bora na la manufaa kwa taifa...;
 
Back
Top Bottom