Nishati safi ya kupikia: Wengi wanatamani kuanza kutumia gesi lakini hawawezi

Nishati safi ya kupikia: Wengi wanatamani kuanza kutumia gesi lakini hawawezi

Kelvin chami

New Member
Joined
Sep 10, 2024
Posts
1
Reaction score
0
Tanzania inaweka juhudi kubwa kwenye kuhamasisha matumizi ya nishati safi ambayo inalinda mazingira lakini pia afya ya wanawake na watoto ambao wanaathirika zaidi na matumizi ya nishati ambazo sio rafiki kwa mazingira na afya.

Hapa naongelea mkaa, na kuni lakini hata hivyo kwa maeneo ya mijini tayari limekuwa swala la kawaida kutumia nishati safi maharani gas ya LPG, huku maeneo ya vijijini yakibaki nyuma sana kwenye kupokea matumizi ya gas ambayo inaonekana kuwa njia rahisi zaidi ya kufikia malengo ya kuwa na vijiji visivyo na moshi kwako mdau.

Mimi nadhani moja ya kikwazo kikubwa ni uchumi ambapo wengi wanatamani kuanza kutumia gas lakini hawawezi kuafford gharama yake japo sikatai kuna swala la watu kushindwa kuadopt matumizi ya nishati hyo na mitazamo kinzani. Je, kwenye swala la uchumi tukianzisha vikoba endelevu kwaajili ya hilo tatizo la uchumi haitasaidia? Kwa maana kwamba.

Waungane watu 25 wachangie 2,000 kwa siku ambapo kwa siku 25 kila mmoja atakuwa kapata mtungi wa gesi na hzo siku tano zinazobakia hela yao inakuwa akiba ya kupunguza gharama mwezi ujao , hata hvyo wakishakuwa na mitungi away zinazofuata watatakiwa kuchangia shilling 1000 tu ndani ya mwezi huo japo utofauti wa matumizi unaweza kuwa kikwazo kwenye hili lakini lengo ni hzo siku tano zinazobakia wanaweza kupunguza gharama hapo baadae.

Kwako mdau hili limescale?
 
Back
Top Bottom