Nishauri Chochote kati ya haya, nimemaliza chuo

nenda kajifunze udereva wa malori makubwa
 
Unasubili nini sasa???

Don't think just do it

Green light ✅SEPA
Ahsante sana kaka ndio maana nikahitaji mawazo Yako...

Hiyo kazi ni ya ulinzi
Mshahara 1.2m kwa mwezi
Kula Bure
Kulala Bure
Usafiri Bure

Renewable contract baada ya miaka miwili.

Sasa nataka Ndani ya miaka hii miwiili nitengeneze connection na watu wa kimataifa then after nitafute jimama la kizunguuu niende nalo ulaya

Alafu mwisho wa siku nataka kufanya biashara either ya kutoa raw materials huku kupeleka kule au kutoa bidhaa kule kuleta huku.

Kwanini mama la kizungu kwasababu ya hafueni ya maisha na kupata makataratasi
 
Kutoboa rahisi kuingia Ngumu
Au una ushauri Gani juu ya njia nyepesi kuingia USA
Ndugu yangu nunua kiwanja Tanzania omba visitors Visa. Kuwaonyesha document unamiliki kiwanja na uns pesa kiasi kwa account unapata. Ukishaingia anza mara moja process ya kuibadili visitors Visa kuwa ya kazi.
 
Nenda veta shinyanga soma course ya kuoperate mitambo ya migodini, baada ya hapo nenda south africa kuna course ya wiki 2 ada yake ni kama laki 8 ya bongo utakuwa certified kama operator wa kimataifa, then kazi ni nyingi Canada, Australia hata GGM unapata chap.
 
Madereva wa malori waliozoea kuendesha scania 113 walibebwa hapa wakapelekwa Dubai kwa kazi ya kuendesha gari kufika kule wakakuta malori ya kisasa yenye mifumo ya ESC,BSM, LDWS , wakashindwa kupiga hata starter kwenye gari wanauliza ufunguo unaingizwa wapi.

Wakaanza kusema wao wamezoea kuvunja mihogo kwenye scania 113 brake hadi turnboy aweke kipisi cha gogo, kwahiyo wameshindwa kazi wamerudi Tz na wewe kuwa makini kabla hujaenda fanya utafiti ujiandae kule hamna kazi ya kubeba gunia mgongoni
 
Jipe mda hata wa miezi 3 ushauri utakaopata utakuwa based na experience na expectations za watu ambaye siyo wewe .
Cha msingi wewe ukikaa na ukaona unataka kuchagua njia ipi itakuwa vizuri zaidi ,kingine pressure kwenye jamii zisikupelepe, be calm
 
Weka hiyo hela kiasi bank
Nenda chuo cha Ufundi kajifunze fundi bomba na umeme kwa pamoja.

Vijana wa leo wana skills ila ukiwapa kazi wanajivuta sana na ujanja ujanja mwingi
Wengi wavivu mno.

Kama ukifanya kwa ustadi mkubwa ukawa na tools za uhakika na ukafanya kwa uaminifu mbona utatoboa popote hata Ulaya?

Unajua kupaka rangi chumba 🇬🇧 ni kuanzia 1.5mya bongo mpaka 3.6m
Inategemea ukubwa wa chumba na area yenyewe

Kutengeneza choo tu kuvunja na kuweka Tiles, Sink na toilet seat pamoja na mabomba na taa peke yako Unalipwa 10m ya bongo.

Nimetengenezewa kwa bei hiyo na vifaa vyote nimenunua mimi.

Jamaa kalipua kwa siku 8 tu peke yake.

Yaani anakula hela zaidi ya Dr
Dunia ya leo inataka uwe na ujuzi ndio utatoboa
 
Huu ushauri mzuri ila sijui nianzie wapi
 
Jipe mda hata wa miezi 3 ushauri utakaopata utakuwa based na experience na expectations za watu ambaye siyo wewe .
Cha msingi wewe ukikaa na ukaona unataka kuchagua njia ipi itakuwa vizuri zaidi ,kingine pressure kwenye jamii zisikupelepe, be calm
Ushauri mzuri sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…