Nishauri juu ya Tiles nisifanye makosa ya kawaida yanayoweza kuepukika

Going Concern

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2011
Posts
1,071
Reaction score
1,212
Habari wakuu! Nimerudi tena baada ya kujikusanya na kujipanga sana. Nimefika hatua ya kuweka vigae (tiles). Sasa kuna jambo ambalo nimejaribu kupitia post mbalimbali na kugundua kwamba vigae pia vina daraja (grades) tofauti, yaani A, B, C.

Kutokana na bajeti yangu, sioni uwezekano wa kutumia vigae vya Kihispania. Badala yake, nimevutiwa na vigae vya India na Dubai. Hata hivyo, nina wasiwasi kwamba nikichagua vigae vya India, je, sito kua nimepata ubora ule ule ambao ningepata kwa kutumia vigae vya Twyford ila huku kwingine nimenunua jina tu?

Pili, ningependa kujua ni sehemu gani au maduka gani naweza kupata vigae kwa bei rafiki.

Mwisho, ni namna gani naweza kujua ubora wa vigae (grades) katika kampuni yoyote nitakayochagua?

NB: Kama kuna fundi mzuri wa kuweka vigae mwenye bei nafuu na sio Bei za DP World, tafadhali nipe ujumbe binafsi (PM) ili tuweze kukutana Jumamosi Goba.
 
Ngoja waje kukupa muongozo,

CC Mahondaw
 
Kwa tiles za India, Egypt etc. Nenda Taha Ceramics. Showroom yao ya pale Africana ndio iko vizuri ina nafasi kubwa utachagua tiles kwa uhuru zaidi kuliko kariakoo ambapo ni panogo. Pia tiles za spain kuna hawa ABC Emporio wana za bei rafiki au unaweza bahatika wakawa kwenye sale ukapata kwa bei nzuri
 
bei zao zina-range ngapi kwa square meter?
 
Shikamoo Ujenzi🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌🙌
 
Umetumia muda wako kabisa kujibu hivi? Ungekaa kimya Hakuna ambacho ungepoteza.
Na ww usingesoma hii comment hakuna kitu ungepoteza. Tatizo mnatakaga watu wawe na mawazo Sawa hakutakua na changamoto. Kupitia comment yangu yupo anayeweza nakshi nyumba yake kwa mawe na ikawa safi. USIKARIRI MAISHA .
 
Na ww usingesoma hii comment hakuna kitu ungepoteza. Tatizo mnatakaga watu wawe na mawazo Sawa hakutakua na changamoto. Kupitia comment yangu yupo anayeweza nakshi nyumba yake kwa mawe na ikawa safi. USIKARIRI MAISHA .
Mkuu una picha hapo, tuone hayo mawe yanavokaa.
 
Nataka kuona linavokaa likitumika kama mbadala wa tiles, huenda unapoint.
Hata sina point mkuu mm ni miyeyusho nyumba yenyewe sina hayo mawe nitajuaje kama yanakaa vizuri. Labda nikupigie picha ya mawe yakiwa mtoni
 
Acha uvivu na kupenda kutafuniwa kila kitu, almost kila kampuni inayojielewa na kufanya biashara makini wana website, page za social media etc.. Sasa wewe ushindwe kwenda kuangalia huko uwaulize wenyewe unataka uambie kila kitu?

tatizo lako unaamini katika 'perfect competition', ingekuwa kila mtu ana fikra kama zako kusingekuwa na kupeana taarifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…