Nishaurini jamani! Mapenzi yamenipa mgongo!!

Safhat

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2012
Posts
270
Reaction score
25
Ni miaka sita sasa tangu niishi na mpenz wangu ninaempenda kwa dhati.lakini naona ameanza kunibadilikia.ni kawaida yetu kuonana kila weekend.lakini cku hizi hana mda wa kuonana na mm,cmu akinipigia kwa wiki mara moja au mbili na huwa hana stori ni salamu tu.nikijaribu kumtilia stori za kimahaba huwa hayupo interested wala haonyeshi furaha yoyote.
Nikimpigia cmu hapokei,nikimuuliz a kulikoni anasema yuko bize na kazi.nikimhoji kama nimemkosea au kuna tatizo lolote anasema hapana.
Kwa kweli ananichanganya na kunikosesha raha coz kashanitambulisha kwa wazazi wake na nyumbani anajulikana.nikimwambia umechange ananifokea.WANAJAMII NISHAURINI..
 
We si ungeshukuru, angalau anakupigia simu kwa week mara moja :cool2:
 
duh...Napenda pesa lakini sio feki.....
 
Mkalishe kitako na umuulize nini kinamsumbua
Labda ameona mapenzi yenu hayana dira wala mwelekeo
Miaka 6 si haba angalau kungekuwa na matumaini ya neema huko mbeleni
 
itakua kuna mtu anamchanganya si bure
mchunguze tu au nenda kwake siku wk end bila kumuambia
 
Hayo mapenzi ya kichina! Najua unaweza kujifariji kuwa kuna watu wanakaa hivyo hata miaka 10. Yaani miaka sita 'mnapendana' upendo ambao hauna nguvu ya kuwafanya muishi pamoja! Ukiulizwa hiyo ni desturi ya wapi?! Unajua kizazi hiki tunajidai wajanja kuliko wazazi wetu lkn ukweli ni kuwa tuko watupu sana, hatuna lolote.
 

Mhhh, hapo penye bold pamenichanganya kidogo, miaka sita unaishi naye halafu hapo hapo tena mnaonana naye kila weekend, maana ya kuishi pamoja si ni kuwa mnaishi nyumba moja na kuonana kila siku?!

Anyway, back to mada yako, ki ukweli muda uliokaa naye kwenye huo uchumba wa kuonana kila weekend ni mrefu sana. Ktk hali ya kawaida, nilitegemea labda mngekuwa kwenye mipango ya ndoa au mmefunga ndoa kabisa ..., Kwa ushauri ni vizuri uzitafakari njia zako wapi ulikosea, na pia kuanza uchunguzi wa nini sababu ya yeye kupunguza mapenzi kwako kama ni kweli ubize wa kazi au kidudu mtu kimeshavamia penzi lenu! Ni vzr pia kujihoji sababu na hatma ya uchumba wenu wa miaka sita kinaga ubaga ili mdogo wangu usiendelee kuinvest penzi na muda wako sehemu ambayo hutaweza kula matunda yake. Ikibidi, shirikisha rafiki zake wa karibu waaminifu huenda watakusaidia kujua tatizo ni nini! Kama si wa kueleweka, waache, watavuraga zaidi mahusiano yako na endeleza uchunguzi wewe mwenyewe.

Pole kwa hilo.

HP
 
Mulika Mwizi, pia jipe moyo, kama Mungu hajapanga muishi wote hatakuoa kwa sababu yoyote ile. Vyovyote vile Mungu anakutakia mema!

Kujihakikishia kama bado unapendwa omba kukaa kwake wiki uone atakavyo kufukuzia mbali.

Ila namuonea huruma nae pia maana atakapokuacha baada ya miaka 2 atajutia uamuzi.

Mpende kiasi, anaefaa kupendwa sana ni Mumeo, sio mchumba!
 
Reactions: LD

mdau umenena,,,kama ipo ipo tu,haya mambo bhana hayana sababu ya kulazimisha saaaana
 
Reactions: LD
Haya mapenzi haya......aaaaargh!!!!!

Kabla ya kuoa niliamini kuwa na mpenzi mmoja ni kutafuta presha!, kumbe kuwa na wengi nayo pia ni presha!

Mila ya wahindi naikubali, hakuna kijana anaejitafutia mke. ni kazi ya wazazi, baada ya kuoa, unaendelea kuishi na wazazi kama kawa!, haijalishi una hela au huna. Na takwimu zinaonesha ndoa zao zinadumu kuliko wengine wote duniani. Tuirudie mila hii ya Mwafrica iliyopotea.
 
si uende nyumbani kwao ukamsemee kwa wazazi wake, kuwa yupo karibu kukutosa
 
si uende nyumbani kwao ukamsemee kwa wazazi wake, kuwa yupo karibu kukutosa

Umenichekesha sana Ndugu, kwani wazazi wake walikiwepo wakati wanaombana kuwa wapenzi? Ha ha haaaaaaaa!!
 

Hapo ndo panahusu vngnezo presha za mapenz ztapasua mishpa ya faham
 
We mwanzisha sredi ni he/she?

Kama ni she basi STUKA!!
Kama ni he ndugu yangu ukiona manyoya ujue....
 

kutambulishwa kwa wazazi siku hizi imekua fashion wazazi wenyewe ndo hawa wa siku hizi mmmh...ila pole mumie wala hilo la kutambulishwa lisikupe shida...cha msingi usome alama za nyakati mapemaaaaa na ujue nn kinaendelea kuliko kuendelea kujiumiza roho tuu......investigate n take action mapema mambo ya kusema ooooh tumekaa miaka mingi now days haina mashiko.....pole n take a good care of yaself....cheers
 
miaka sita?duh sio nakukatisha tamaa,ila huyo mtu hana nia ya kuishi na wewe,maana miaka sita kwa watu wenya nia kinekuwa kimeeleweka.

note:uchumba wa mda mrefu unaeffect kubwa sana maana wewe umeweka 100% kuw aupo nae milele lakini lwenzio kashakutoa vikasor kibao ndo maana siku hizi anaona huna maana tena.

Muombe Mungu akujibu,shida moja ,watu huwa hatukubali majibu ya mungu hasa yanapokuwa tofauti na tunavyotaka,ila nakushauri kubali lolote litakalotokea,maana its for your own good.
polee sana maana inauma unaweza pasuka moyo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…