Nishaurini mafuta mazuri kwa mke wangu

Desteo

JF-Expert Member
Joined
Jul 27, 2011
Posts
494
Reaction score
123
Wife ngozi yake ni delicate sana. Vitu vya jamii ya chuma vinamdhuru kwa kuwashwa na kuota vipele. Poda yenyewe inamsababishia chunusi. Kwa sasa hatumii mafuta yoyote hasa usoni kwani ngozi yake ni ya mafuta pia. Napenda kumwona akiwa na uso mwororo usio na chunusi ila ana hiyo changamoto ya kuharibika ngozi akitumia baadhi ya vipodozi.

Ushauri wenu tafadhali ili na yeye awe na ngozi soft. Atumie vipodozi vya aina gani
 
Mmhh mwambie ajaribu kupaka mafuta ya Nazi na sabuni ambayo atatumia kunawia uso hata kuogea iwe zile za magadi.. Zile za bluu na nyeupe iviii nadhani sokoni zinapatikana kwa urahisi ..... Ni vitu vya gharama nafuu na pia zinaweza zikamsaidia mwambie ajaribu na hiyo....
 
Mawese
 
Za magadi si ndio zinazidisha kupausha ngozi?
 
Anza kwanza kwa kutoa chunusi alizonazo kwa kutumia hii
Kwa tsh 10,000 tu utaondoa tatizo hilo then likishaisha tuangalie aina ya ngozi yake then atapata lotion inayomfaa nichek 0714547830
 
mtafutie hiyo hapo ni nzuri shemu wako pia alikuwa anasumbuliwa na chunusi kama ulivyoelezea

 
Mafuta ya nazi hayafai kwa ngozi ya mtu mwenye mafuta sababu yatamuongezea mafuta zaidi.
 
Napaka mafuta yangu ya nazi na yananifanya ngozi yangu kuwa nyororo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…