Nishaurini: Ndugu yangu alipohitimu chuo mwaka jana akahamia kwangu, nimsaidiaje awe bize? Hana shughuli

Nishaurini: Ndugu yangu alipohitimu chuo mwaka jana akahamia kwangu, nimsaidiaje awe bize? Hana shughuli

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Heri ya mwaka mpya wadau.

Kuna mtoto wa shangazi yangu wa kiume (23) alipomaliza chuo mwaka jana 2020 mwezi wa nane kama sijakosea akaja hapa kwangu maana kashapazoea kwasababu chuo anachosoma kipo sehem nayoishi.

Sasa basi ndio ivyo, kwa sasa dogo hana kazi na ninaelewa kwamba kupata kazi ni ngumu lakini sio kisingizio cha kutokuwa na shughuli yoyote, yani akimaliza kazi zile za asubuhi wakati nipo, mimi na wife tukiondoka kwenda job hana shughuli nyingine.

Muda mwingi yupo na simu akisikiliza mziki na kuchat au kucheki mambo ya Insta.

House girl kanipa taarifa tunapokuwa tumeenda kazini mara nyingi marafiki zake wanashinda hapa na kula hapo hapo hadi jioni, watapiga picha zao, kupiga story na hata kuhamishia chumbani kwake game niliyowanunulia watoto wawe wanaichezea weekend (play station 4)

Pia house girl baada ya kumbana, kaniambia huwa anaingiza madem getoni kwake, yeye hakai nyumba kuu anakaa zile za nje, hicho chumba nilitaka kiwe stoo zaidi ya hapo ni mtu wa kushinda sana kitaa.

Kurudi kwao ni ngumu kidogo maana ni vijijini huko, shangazi kaniomba abaki huku huku maana ni mjini na angalau kwa mbali huwa kuna matangazo ya kazi au hata connection.

Nifanye nini awe busy wakuu.
 
Kazi zipo nyingi tu, sema Ajira ndo changamoto.

Mpatie mtaji hata wa laki mbili mwambie Auze maji maeneo ya Stand na aache fikra za kwamba kazi ni zile za ofsini tu,
Failure to do so, rudisha kijijini.
 
Mnunulie ile mzani ya kupimia uzito azunguke mitaani kupima watu atapata hela.
 
Me nadhani kaa nae kiume ongea nae. Man to Man.
 
Mnunulie ile mzani ya kupimia uzito azunguke mitaani kupima watu atapata hela
Mpatie mtaji hata wa laki mbili mwambie Auze maji maeneo ya Stand na aache fikra za kwamba kazi ni zile za ofsini tu,
Failure to do so,rudisha kijijini
Hio itakuwa ngumu kidogo, si unawajua tena madogo hawa wakimalizaga chuo hwajakaa kitaa hata mwaka bado wanakuwa na hope ya kupata kazi safi 😂😂

Ila ntajaribu kumwambia , asante kwa ushauri
 
Biashara ya chakula haimtupi mtu, ajifunze kupika maandazi kupitia you tube. Siku ya kwanza apike 1/4 kilo mle wenyewe. Akijua vizuri tafuteni hoteli ya kupeleka.

Kuna kaka alitoa ushuhuda kanisani. Yeye alimuoa girl friend wake wa chuo. Mdada amegraduate tu na ajira mkononi. Hawakusita kuendelea na mipango yao ya harusi mkaka akisaidiwa na ndugu.

Baada ya ndoa akawa house husband. Anasema mke wake hakuwahi kumnyanyasa lakini akiwa kama mwanaume alikua anajisikia vibaya sana.

Walikua na bread maker walipewa kama zawadi ya harusi. Alianzia kukandia unga. Alianza na kilo mbili za unga, alikata maandazi akapelela maofisini watu wananunua kwa breakfast wengine lunch. Mwisho alikua anapata order za party weekends.

Ni kutokana na maandazi alipata connection ya ajira ya taaluma yake.
 
Back
Top Bottom