Nishaurini Ndugu zangu juu ya huyu mwanamke

Pamoja na hayo alichojibu baada ya kumtaka kumfahamu anawasiliana na nani ni hiki:
1. Huna haja ya kufaham marafiki zangu
2. Huyu nilianza nae mahusiano kabla yako
3. Nina uwezo wa kuwa hata na wanaume 10 ni maisha yangu.
Kwa majibu hayo bado unauliza cha kufanya?!!

Huyo ana waume zake wanaomfikisha, wewe ni mchepuko usio na umuhimu
 
Yaani bado unatafuta ushauri?. Ubongo wako umeumbwa na nini?
 
Dogo. Jikite kwenye kuhangaikia maisha na uwasaidie wadogo zako na Mama yako aliyekulea.

Sasa hapo unataka tukushauri nini ambacho hujaelewa.

Wanawake hata akiachwa kwa marungu ngumi na mateke huwa haachi kuhifadhi namba za X wake. Hiyo ni Big No.
Atajiapiza hadi kwa Mungu na mbele ya Dunia kwamba hana mawasiliano nao. Usiamini.

Alianza kukwambia ukweli kuwa ana watatu. Na mkawekeana mipango kuwa hatarudiana nao.

Leo anakwambia huna haja ya kuwajua na hata akiwa nao 10 hayakuhusu.

Wewe bado unataka ushauri?
 
Achana nae Achana nae, Achana nae...usije baada ya miaka miwili ukarudi hapa unatia huruma, dalili umeziona hivyo basi kama unajifanya una huruma sana basi huruma yako itakuponza, naamini Kwa hisia zangu level of your emotional intelligence Iko ya kuridhisha, don't be a stupid.
 
Piga chini utalea watoto sio wako bora mwanaume usiwe mwaminifu ila mwanamke siemwaminifu ni hatari kwa ndoa.
 
Yaani chuoni ulifuata nini?
Tuanzie hapo kwanza.
 
Yani umekutana na mwanachama wa UWT yani mdogo wa merry chatanda
 
mwambie unampenda na unataka kumuoa,hivyo aache hayo mawasiliano yote ya zamani,vinginevyo utamuacha utafute mwingine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…