DOGO bana, we una miaka 21 na demu wako ana miaka 24!!! mwenzako keshakomaa wakati ww bado utoto unakusumbua na hivyo anaamua tu kukuchezea kisaikolojia...angalia unavyotapatapa wakati issue ni simple sana ! Na wewe mchezee kisaikolojia like this, kwanza uchune kama cku 3 hivi bila kukol wala nini...ingawaje am afraid kama utaweza. Na ukiweza, cku ya tatu tafuta jina la msichana linalofanana na jina la msichana wako. Assume gal wako anaitwa fatma; wewe andika msg kama hii "am sorry fat'hiya, let's cancel the trip untill next weekend. By da way, nimeona ni much better for zanzibar than bagamoyo...!" ukishamaliza, send hii msg kwa gal wako na yeye picha atakayopata ni kwamba umekosea kumtumia yeye na uliyemkusudia ni FAT'HIYA lakini ulituma kwake kv FATMA na FAT'HIYA ni majina yanayoongozana kwenye phonebook, na kwakuwa haukuwa makini ndo maana ukatuma kwake (fatma) badala ya kwa fat'hiya!! Kama mpenzi wako bado anakupenda, atatumia kama dakika tatu hivi kui-digest hiyo msg na baada ya kushindwa kuvumilia, ataenda hewani ama kwa kupiga au ku-beep ili apate ufafanuzi! Hata akipiga, usipokee, na badala yake kata kisha tuma msg hii "nani mwenzangu? can't talk coz' niko kwenye gari....!" Nakuambia, hapo atafura kwa hasira na kisirani mithili ya mbogo majeruhi! shenzi taipu, umefuta namba yake halafu una mipango na hawala yako fat'hiya ya kwenda unguja?!hilo ndilo atakalowaza! What next, kama bado anakupenda, lazima atie maguu gheto huku akiamini anakuja kuvuruga mipango yako na fat'hiya bila ya kujua kwamba ndo anajileta mwenyewe kwenye tundu! Asipo-react, pamoja na kumtia mavivu kote huko, basi fahamu kwamba, hapo huna chako mpwa, na hapo utatakiwa kufanya ONE of the TWO decision making. Kujisogeza pembeni taratibu (usiache kwa mbwembwe, utaona aibu siku ukitaka kurudi tena) au usubiri kupewa cha mbavu kwani nafahamu kwamba baadhi ya watu wao raha yao ni kuachwa....yenyewe mpaka ipigwe chini kwa maudhi ndipo ijue kwamba kweli haitakiwi. Ukiwaambia, utawasikia, hujawahi kupenda; stupid...wewe umezaliwa nae huyo!