Nishaurini, nisome nini?

Nishaurini, nisome nini?

Rasasem

Senior Member
Joined
Jun 25, 2022
Posts
100
Reaction score
79
Habari waungwana,

Poleni na hongereni kwa majukumu ya kulijenga Taifa, niokoe muda ili nisiwachoshe ndugu zangu, kitaaluma mimi ni mwalimu na tayari nina diploma ya physical education ambayo nilisoma nikiwa tayari nimeajiriwa lakini mpaka sasa haijanipa kile nilichokitaka.

Kwasasa nataka kujiendeleza ngazi ya shahada hivyo naomba mnishauri ni kipi nikasome kwa kuangalia umuhimu wa kozi hizi "Bachelor of physical education and sports science kulinganisha na kozi nyingine za degree za ualimu?

Natanguliza shukrani toka huku kijijini!
 
Back
Top Bottom