Nisome kozi gani yenye soko la ajira?

Joined
Jul 8, 2022
Posts
18
Reaction score
18
Habari wanajukwaa,

Nimemaliza kidato cha sita mwaka huu tahasusi ya PCB na nimepata DIV two ya 12 nikiwa na physics D, Chemistry D, Biology D, Bam D, na Gs D

Nipo njia panda kwa sasa juu ya kitu gani nisomee chuo kikuu ukizingatia ufaulu mkubwa wa mwaka huu kozi kama Pharmacy, MD, Medical Lab, na Nursing.

Zina compitation kubwa saana naombeni ushauri wenu katika kozi zingine ambazo nina vigezo vya kusomea zenye soko la ajira.

Na nikisoma kozi hizo nitafanya kazi gani baadae

Naombeni ushauri wenu wakubwa wangu asanteni

Mungu awabariki.
 
kwanza hongera, pili kwasasa we ukiaamua kusoma chochote we soma tu acha kabisa kuwaza ajira maana hata hao MD wana hustle sana ingiwa sio kama wengine but hustle ipo pale pale kwa kozi yoyote ilee kijana wetu, but kuna kozi nyingi pale SUA, UDOM hata KCMC unaweza kuaangalia.
 
Diploma ya computer science kama una hobbie ya mitandaoni na electronics. Pia nadhani ndiko Dunia inakoelekea hata ukija kosa ajira ukiwa wa kujiongeza utafanikiwa.
 
Bitter truth, huwezi pata MD, Nursing, pharmacy, wala Lab Kwa huo ufaulu hata kama ni kampala..omba BVM, FOOD SCIENCE, ANIMAL SCIENCE. Utanishukuru badae
 
Bitter truth..huwezi pata MD,Nursing,pharmacy,wala Lab Kwa huo ufaulu hata kama ni kampala..omba BVM,FOOD SCIENCE,ANIMAL SCIENCE..utanishukuru badae
Na mnavyo penda kupewa shukurani Sasa!!!

Kwanini asimshukuru Mungu?
 
Amua tu.... yaani Angalia akili yako inasemaje
 
Omba MD ndugu, Ila isiwe muhimbili. Jaribu kuomba Udom, Kcmc, Bugando, nk. Utapata, usiogope
 
Kuna uhaba wa walimu wa Sayansi. Komaa na ualimu ya huko baadae utajua mbele kwa mbele....

Usisahau Nyerere, Mwinyi na Magufuli walikuwa walimu....

Nitakupa kura yangu
 
Hongera janja Kwa matokeo mazuri ingawa yanaweza yasifue dafu katika course nyingi za Afya kulingana na ufaulu ulivo ila bado haiondoi ukweli kuwa umejitahidi sana

Turudi kwenye mada, kama Kaka yako, nakushauri omba Kwanza course ambazo wewe unazipenda ili ata kama ukija kukosa Ajira basi usiwe na majuto mawili mawili

Baada ya hizo course, sasa nakushauri kulingana na mtaa unahitaji nini kulingana na uelewa wangu, Pale SUA omba course hizi, Horticulture, General Agriculture,BVM na kamwe narudia tena kamwe usiombe Animal Science, kisha Nenda pale Mlimani malizia course ya Beekeeping

Hizo course zote utakuwa na nafasi kubwa ya kupata mkopo maana zote zipo kwenye kundi la priority unless labda history yako ya shule ulizosoma ikutupe, ukipata mkopo tumia vizuri na utunze maana ndio utakuja kuwa mkombozi pale tu utakapomaliza chuo
 
Bam D? Na GsD? Na sio S?

 
Shukran saaaaan
 
Nakushauri soma political science ukimaliza nenda kaombe kazi ya kupiga domo pale Lumumba.
Ukiwa unasoma anza kuwa chawa kwa viongozi wako wa chama na serikali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…