Nisome kozi gani yenye soko la ajira?

Kapige Tax na kozi zinazofanana na maswala ya fedha..utasota Ila siku ukibutua no Boomm u alamba asali.
 
Nilimsikia Paskal Mayalla akisema ati course ya sheria ndio rahisi kuliko zote, nenda huko uhalifu hautokaa uishe Bongoland.
Nauli ya wakili kwenda mahakamani ni 50,000/= kila tarehe ya case.
 
Hata usome hadi mwisho wa kitabu ajira ni wazanzibar tu kwasasa,,
 

Wewe inaonyesha ni muongo, tangu lini BAM na GS zikawa na principal pass zaidi ya S kwa yeyote aliyefaulu?
 
Kama unahisi huna cha kunishauri ni bora ukae kimya tu
Hajafafanua tu ni course gani but trust me kama una hobbie ya hivo vitu ukaja Soma course yake (sijui ni computer science or computer engineering au au VETA huko sijui Sina hakika ) huhitaji kuajiliwa na utakuwa unatengeneza kipato kizuri kisicho na Makato mengi, wakati mwingine zaidi ya wafanyakazi wa level ya degree wengi tu.
Note: kwenye hivo vitu uwe expert mzuri na watu wakuamini, na uwe na hobbie ya hivo vitu. Ila kama unasomea ajira ok pambana huko ujaribu bahati Yako pia
 
Nenda lumumba ofisi ndogo watakupa ushauri ukasomee nini.

Nasikia kuna kozi mpya inaanza mwaka huu inaitwa bachelor degree in uchawa pro.

Core subjects kusifu na kuabudu,alipo tupo,anaupiga mwingi.

Kila la kheri..na wanatoa grants sio mkopo.

#MaendeleoHayanaChama
 
Haaaahaaaaahaaaaa umenivunja mbavu
 
Bitter truth, huwezi pata MD, Nursing, pharmacy, wala Lab Kwa huo ufaulu hata kama ni kampala..omba BVM, FOOD SCIENCE, ANIMAL SCIENCE. Utanishukuru badae
BVM huwezi kupata kwa huo ufaulu.Aombe ualimu atakuja kunishukuru baadae.
 
Kasome chuo cha uvuvi mbegani... utanishukuru baadae⁶
 
UALIMU UALIMU UALIMU. Una physics so ukisoma ualimu suala la ajira kwako ni Kitongaa. utakuwa unatushangaa ma jobless imekuwaje hatuna ajira.
 
Check www.tcu.go.tz download Undergraduate Admission Guidebook Guidebook inaonyesha vyuo na kozi zao na sifa za kujiunga kwa kila kozi...utakuta kozi nyingi sana ambazo unasifa chagua unayotaka kushi katume maombi..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…