Scania complete bus mfano scania f95_310hb au f94_310hb zenye gearbox ya gia sita ziko vizuri sana hususani hizi scania f95_310 euro iii emission piston tano unywaji wake mafuta ni kidogo sana kuliko scania za piston 6 zipo vizuri kwenye milima,tambarare,na barabara korofi hata safari ndefu zinaenda bila tatizo lolote ila ukizembea kwenye service zinasumbua sana kwa kuwa zinatumi mfumo wa umeme kwa asilimia kubwa matengenezo yake hufanyika kwenye matawi ya sab scania,Nissan Diesel kwa injini mbele toleo la mwisho ni hizi cb46 ambazo zilikuwa kwa Sumry,taqwa,falcon,nk hizi injini yake ni euro ii emission standard zinavumilia kutembea umbali mrefu kama kama 1000km kwa siku na ikapumzishwa maana hizi ikifululiza safari ndefu bila kupumzishwa huwa zinaibua magonjwa mfululizo na zinakunywa sana mafuta hasa zikianza kuchoka au pampu yake ikiguswa ili iwe inakimbia zaidi vile vile Nissan ikiwa na diff la high speed inakimbia sana tambarare,kwenye miteremko,barabara korofi,na inapanda taratibu sana mlima lakini ikiwa na diff la low speed inapanda sana mlimani lakini haiwezi kukimbia sehemu yoyote tofauti na mlima na kwa sasa uzalishwaji wa Nissan Diesel kwa ajili ya mabasi ya injini mbele umesitishwa